Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
MIHOGO YA NAZI Mahitaji Mihogo mikubwa 2 Nazi kubwa 1 Chumvi Pilipili manga kidogo. Maji Njia Chukuwa mihogo yako menya na kata kata vipande kisha kuna nazi yako na tengeneza matui matatu. Kisha chukuwa sufuria weka mihogo,chumvi na pilipili manga na kisha weka tui la tatu na la pili kwy mihogo mpk ifunike mihogo ikipelea ongeza maji kidogo acha ichemke mpk mihogo iive kabisa kisha weka tu la kwanza na acha kidogo ichemkee na tayari kwa kuliwa