Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ukikutana na mtu barabarani akakuuliza kama una rafiki wa kweli utaweza kumjibu kama ndiyo au hapana?

Hapana shaka utasita kumjibu, huenda hutaweza kupata jibu moja kwa moja na kama utaweza kumjibu mara tu atakapokuuliza, utakuwa una bahati sana.

Hili ni moja kati ya matatizo ya maisha. Tunapata marafiki wengi, lakini tunashindwa kuwafanya kuwa marafiki zetu wakati wote, hata wakawa marafiki wa kweli.
 
Kwa hakika tunahitaji kuwa na marafiki katika maisha yetu kwa sababu ndiyo wanaotupenda na kutujali. Ni washirika wetu katika raha na shida, furaha na huzuni, tabu na raha, njaa na shibe, umaskini na utajiri, ugonjwa na afya na pengine hata katika uzima na kifo na mengineyo mengi. Husemwa kuwa na marafiki wema na wa kweli hushinda kuwa na mali.
 
Sasa hebu turudi tulikoanzia. Acha swali la marafiki wa kweli kwa muda, ili tujiulize swali jingine. Je, ukiwaorodhesha marafiki zako wote wanaweza kufikia wangapi?

Je kama ungefariki leo, unafikiri ni marafiki zako wangapi wangefika kwenye msiba wako? Kama ni wachache sana bado unahitaji kutafuta marafiki.

Nina hakika kila mmoja wetu ana marafiki aliowapata katika nyakati mbalimbali za maisha. Lakini pengine kuna wengi tuliowapoteza.
 
Back
Top Bottom