Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

NAKULA CHOCHOTE
Baada ya kubembelezwa sana unamtoa mdada ‘out’, mnaenda sehemu mmekaa.
Wewe: Ehe utakula nini switii?
Mdada: Chochote
Wewe: Nikuagizie ice cream
Mdada: Hapana meno yanauma
Wewe: Haya wacha walete chips kuku
Mdada: Jamani kila siku chips kuku leo tubadilishe
Wewe: Toa wazo basi unataka kula nini
Mdada: Chochote
 
Hahahahaha kazi kwelikweli, juzijuzi kazini kwetu kulitangazwa semina ya siku moja ya wanaume waliooa. Kuna taasisi inayohusika na jinsi ya kuendeleza familia zenye Amani, ilifika kazini kwetu na kututangazia kuwa wanaume wote walio katika ndoa wahudhurie semina bila kukosa, bosi wetu akajitolea kulipia chai na chakula cha mchana. Hii ishu sikutaka inipite, kwanza nilikuwa na maswali mengi sana nilitaka kujua jinsi ya kurudisha penzi la awali na mke wangu, nilitaka mambo yarudie enzi zile ambapo kila niliporudi nyumbani nilikuta katandika kitanda vizuri na juu yake kaweka maua
 
Nilikuwa nakuta chakula kimefunikwa kawa lenye maneno matamu ya mahaba. Nikitoka kidogo hata kama nilienda mtaa wa pili kucheza bao, nikirudi namkuta waif kabadili nguo ananikaribisha utadhani nilisafiri wiki. Nilikuwa natamani enzi zile zirudi tena

Basi semina ilianza kwa maelezo mengi na mifano mingi sana. Mchana baada ya kula, kila mtu aliambiwa amtumie mkewe meseji kwenye simu. Meseji rahisi tu, aandike neno NAKUPENDA na kulituma kwa mkewe.
 
Basi kila mtu akaandika na kutuma, baada ya hapo tukaambiwa kila mtu ampe jirani yake simu yake. Haikuchukua muda mrefu milio ya mesej za majibu zikaanza kusikika , watu wote tulikuwa kimya. Kisha muwezeshaji wa semina ile akaomba walioshika simu waanze kusoma majibu yaliyorudi kwenye simu. Ngoma ilianza hapo. Simu ya kwanza ilisomwa jibu lilikuwa, ‘Vipi baba Jeni, kuna nini?’. Iliyofuata,’Labda enzi hizo siyo sasa’, nyingine ikajibu, ‘Sikukopeshi tena huwa hurudishi hela zangu’, nyingine ikarudi imeaandikwa, ‘Umefanya nini tena? Safari hii sikusamehe?’
 
Tulianza kucheka sasa, ikasomwa meseji nyingine mke akajibu,’Sijakuelewa’. Nyingine ikajibu,’Ni wimbo mpya wa Diamond?’, mke wangu nae akajibu, ‘Usiponambia meseji hii ilikuwa inaenda kwa nani, usirudi’. Mwenzangu mmoja akapata swali,’Nani mwenzangu?’ Bosi wetu nae alipata jibu toka kwa mkewe, lilikuwa onyo, ‘Sinilikwambia uache kulewa mchana mume wangu’. Ila kulikuwa na meseji moja ya jamaa yetu wa uhasibu ambaye mnoko sana wakati wa kutulipa mafao yetu, ila tulimuonea huruma alipoanza kutoa machozi kutokana na jibu la mkewe ambaye inaonekana alijichanganya na kujibu,’We vipi nilikwambia usiwe unanitumia meseji za hivi mume wangu akiziona itakuwa shida’ Na simu ya afisa utumishi ilikuwa na swali, ‘Vipi umemjaza mimba mtumishi mwingine?’. Tumetoka kwenye semina tumechanginyikiwa kuliko tulivyoingia.
 
Yaani huwezi amini lakini kilichonitokea wiki iliyopita kimenikosesha amani kabisa, nilikuwa nimepanga wiki hii niwe kijijini kwetu nikiwa na furaha, mambo yako tofauti nabaki nahangaika kujificha ficha kama panya. Kosa ni kampuni ya basi moja isiyo na upeo wa kimaadili. Mwezi mmoja uliopita mama mkwe alikuwa amaekuja kututembelea kutoka kijijini. Alikuwa anaumwa kidogo na pia alikuwa kaja kuwasalimia wajukuu zake.
 
Mambo yalienda vizuri aliweza kupata matibabu na nyumba ikawa na furaha. Sasa sisi ni kati ya watu ambao bado tunaoheshimu mila za Kiafrika, mama mkwe ni mtu anaeheshimika sana na yeye ananiheshimu sana mimi, kimsingi tunajitahidi kukwepana ili heshima iwepo kubwa. Ingekuwa zamani hata kuishi nyumba moja na mama mkwe isingewezekana ingekuwa mwiko. Basi siku za mama mkwe kukaa kwetu zikaisha na tukawa tumepanga wakati anarudi kijijini,
 
turudi wote maana na mimi nilikuwa na kalikizo ka wiki mbili. Pia ingesaidia watoto wakujue kwa bibi yao, wasije wakadhani wao ni wa mjini. Nilikata tiketi mapema ili isije ikatokea mimi na mama mkwe tukalazimishwa kukaa kiti kimoja. Siku ya safari watoto wetu wawili, mke wangu na mama mkwe tukaingia kwenye basi mapema tayari kwa safari ya kwenda kwetu mikoa ya kusini. Mambo yalikuwa safi, kiyoyozi kikawashwa, viti vya mneso na tulipofika Kibaha video zikaanza kuonyeshwa. Sikuwa na hili wala lile nilikuwa nasoma gazeti lakini nikawa nausikia muziki.
 
Back
Top Bottom