Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ghafla nikasikia watoto wangu wanacheka wakaanza kumwabia bibi yao, ‘Bibi bibi ona yule kavaa kichupi kama changu’ Dah nikashtuka, kuangalia naona video kwini ‘anamwaga lazi’. Dah balaa gani tena hii asubuhi mapema hivi, nikakata jicho kumuangalia mke wangu namuona kajifunika kanga usoni anajidai kalala, mama mkwe nae kaficha uso, watoto wanazidi kushangilia, sauti zao ndio zinasikika basi zima, ‘Baba baba angalia likubwa lizima limevaa kichupi’. Dah nikajificha nyuma ya gazeti hata maandishi siyaoni
 
Ukaisha wimbo wa kwanza ukaja mwingine ikawa balaa zaidi, pakukimbilia hakuna kila wimbo wanashindana kumwaga lazi, hata wimbo mtu anaongelea namna ya kupata pesa lakini video inaonyesha vibinti havina nguo za kutosha, basi ikawa adhabu kubwa mpaka tulipofika Morogoro. Kufika Moro, mama mkwe akamuita mke wangu na kumwambia wazi hawezi kusafiri na mkwe kwenye basi moja katika mazingira ya video zile. Nikamuomba konda abadili video akajibu ile ndio wateja wanapenda. Kukawa hakuna jinsi bali mimi nishuke au mama mkwe ashuke, nikashuka mimi na kuruhusu familia itangulie mimi nitafute basi jingine. Basi toka nimefika huku kijijini bado hakuna amani kati yangu na mama mkwe, kila tukikutana tunakwepana, kikwetu kuangalia picha za aina ile pamoja na mama mkwe na watoto si sawa kabisa, lazima mkosi mkubwa utatufikia hata sijui nitumia tambiko gani kufuta uchuro ule
 
Nimetoka kwenye mkutano wa muhimu sana. Mkutano wa siri sana, na kwa kweli tulichoamua kitashtua jamii. Unajua jamii yetu hii, ina watu wakorofi sana, wakiona mtu umenyamaza basi itaanza kukuchokoza inataka useme ukiamua kukaa kimya basi wataendelea kukufanya uonekana fala
 
tumebahatika kuwa na wataalamu wengi tu, najua kwa hapa kwetu nikisema wataalamu kila mtu anafahamu nina maana gani, hawa ni watu ambao wanaweza kufanya mambo ambayo hata wanasayansi wazungu wanabaki wameduwaa hawajui kinachoendelea, wataalamu wetu wanaweza kusafiri kwa ungo wakatoka Dar mpaka Mtwara na kurudi katika muda wa masaa
 
kwanza tulitumia mbinu za kiintelijensia kupeana taarifa kuhusu mkutano huo, baada ya hapo hata ukumbi tulioutumia ulikuwa ni siri kubwa, lakini tumeweza kukamilisha kwa mafanikio makubwa, tulishawahi kusema penye wazee haliharibiki neno.
 
Kwa miaka mingi sisi tumekuwa kimya sana tukiiongoza jamii katika mambo mengi ya msingi na kutoa ushauri ambao umesaidia wakubwa na wadogo, hatukutaka sifa wala kiki, tulitimiza majukumu yetu kiroho safi kama mnavyosema kwa lugha ya siku hizi. Lakini bila sisi kuwachokoza ,
 
ghafla kila mahala mmeanza kutuchokoza, kwenye mitandao mumeweka picha za kejeli, zikisema ohh wahenga wamefanya hili, ohh huyu ndie muhenga aliyesema lile, jamani tumewakosea nini? Sasa tunaliamsha dude, wale walioanzisha utani kwa wahenga, na wale walioendeleza utani kwa wahenga, mjitayarishe, wataalamu
 
wamekwisha ruhusiwa kubuni adhabu, hivyo kama ulikuwa mmoja wapo usishangae asubuhi ukiamka ukakuta umelala bafuni, ni sisi tuliyoleta msemo, ‘akutendae mtende’. Wale waliotuchokoza nawashauri tafuteni wahenga waliojirani mkajisalimishe kwani
 
Back
Top Bottom