Ukaisha wimbo wa kwanza ukaja mwingine ikawa balaa zaidi, pakukimbilia hakuna kila wimbo wanashindana kumwaga lazi, hata wimbo mtu anaongelea namna ya kupata pesa lakini video inaonyesha vibinti havina nguo za kutosha, basi ikawa adhabu kubwa mpaka tulipofika Morogoro. Kufika Moro, mama mkwe akamuita mke wangu na kumwambia wazi hawezi kusafiri na mkwe kwenye basi moja katika mazingira ya video zile. Nikamuomba konda abadili video akajibu ile ndio wateja wanapenda. Kukawa hakuna jinsi bali mimi nishuke au mama mkwe ashuke, nikashuka mimi na kuruhusu familia itangulie mimi nitafute basi jingine. Basi toka nimefika huku kijijini bado hakuna amani kati yangu na mama mkwe, kila tukikutana tunakwepana, kikwetu kuangalia picha za aina ile pamoja na mama mkwe na watoto si sawa kabisa, lazima mkosi mkubwa utatufikia hata sijui nitumia tambiko gani kufuta uchuro ule