Anataja madhara hayo kuwa ni magonjwa ya ufizi yanayojionyesha kwa kutoa harufu mbaya ya kinywa, kutokwa damu katika fizi na kulegea kwa jino au meno na kutoboka kwa meno.
“Ni kweli kuwa matatizo ya meno yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku.
“Hii inatokana na tabia yetu ya ulaji wa mara kwa mara wa vyakula hasa vyenye sukari kama vile soda, biskuti, chai, juisi na uji wenye sukari,” anaeleza Dk Chembele.