Naomba jamii ipate ujumbe huu muhimu ili kuepuka madhara hatari yanayoweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na majibu au saratani,” anasisitiza Dk Chembele na kuongeza kuwa”
“Mbali na dawa hizo za waganga wa tiba asili kusababisha wale waliozitumia kuwa katika hatari ya kupata saratani na majipu, dawa hizi zinazotangazwa kutibu meno bila kung’oa husababisha madhara zaidi kwa kuwa wengi huchelewa kupata tiba stahiki kwa kuamini kuwa wameshapata tiba sahihi kumbe wametiwa ganzi tu ya mishipa ya fahamu.
Anasema ingawa wengi huzinadi dawa hizi lakini ni ukweli ulio wazi kuwa hazijafanyiwa utafiti wa kutosha kuhusu matokeo yake katika jamii na ndiyo sababu kuna uwezekano mkubwa wa kusababisha saratani ya koo na kinywa.