Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

2: FLAGMETIC -Wana uwezo mkubwa kiakili baada ya melancolin -Uwezo wao katika utendaji wa mambo inasemekana ni kati ya asilimia moja na sitini -Ni mabingwa wa kuahirisha mambo (mfano kama akitaka kwenda kupalilia shamba, akafika na kukuta kuwa majani ni -machache atabeba zake jembe na kurudi nyumbani hata kama ni msimu wa kupalilia) -Wanapenda sana kupuuzia mambo ikiwa
 
hawakuyaelewa ama kuyaona kwa macho yao wenyewe -Hawapendi kukubali ama kusifia mafanikio ya wenzao -Ni kundi la watu wabishi sana na ambao ni mahiri wa kujenga hoja kwa jambo wanalolitetea -Katika ushindani hasa wa hoja huwa hawakubali kushindwa kirahisi (anaweza kusema mti ni gari akajenga hoja akazitetea na wote mkakubali hata kama ni kwa shingo upande)
 
Mawakili majaji na mahakimu mahiri duniani ni wale wanaotoka katika kundi hili -Ni watu wanaopenda kutafiti na kufuatilia mambo mbalimbali ndio maana maongezi yao mengi hutawaliwa na mifano na takwimu halisia -Wanapenda kufuatilia mambo ya wengine pasipo hata msingi wowote (wanapenda sana ushushushu) -Wapelelezi mahiri hutoka katika kundi hili -Ni watu wasioumizwa
 
kufanya makosa -Hawapendi kuwaamini wenzao -Ni wepesi wa kupokea lakini ni wagumu wa kutoa ama kujitolea kwa mambo mbalimbali -Wanatafakari mambo kwa kina na kuyatolea uamuzi wa uhakika -Mapenzi (love affairs) si kitu kinachowaumiza sana (kundi linaloongoza kwa kuwa single na ambalo ni rahisi kukubali talaka pale
 
inapotokea migogoro katika ndoa zao) -Wanasamehe haraka sana kwa sababu hawajali (they don’t care) -Ni wagumu wa kuomba msamaha (i.e mara zote hutaka kuonekana kuwa wapo sahihi) ndio maana hupoteza nguvu za Mungu kirahisi (imani zao zikipoa huwa si rahisi sana kuamka) -Ni wagumu wa kupokea mambo mapya hasa yahusuyo imani na sera, vile vile si rahisi kuachana na imani ama sera
 
walizozipokea -Si watu wanaojali muda na ratiba -Ni rahisi kukatisha mahusiano ya aina yeyete pindi wanapogundua kusalitiwa ama kurubuniwa. -Hawaogopi kumkosoa mtu ama kumuumbua hata kama ni hadharani -Hawaumizwi na maneno ya watu dhidi yao -Ni wasuluhishi wazuri wa migogoro ya kijamii na ya kimataifa na wenye ushawishi wa kina (i.e
 
karama ya utele kwa neno la upatanisho ipo kwao) -Ni kundi linalifanya mambo mengi lakini kwa ufanisi wa wastani -Ni kundi la watu ambao sio wakereketwa wa masuala ya usafi na unadhifu (i.e kimavazi na kiutaratibu) -Wakianzisha jambo huweza kuliachia njiani bila kulimaliza na wala wasiumizwe na kukwama huko -Ni watu wasiopenda vurugu hasa demokrasia ya ushuluhishi wa hoja
 
inapokwama -Wapo tayari kusalimisha chochote walicho nacho ilimradi wabakie na amani (wanafahamika kama peace makers) -Watu waliojaa dharau na ambao muda wote huona wao ni bora kuliko wengine katika mambo yote -Hawapendi kuelekezwa na mara nyingi eidha huwadharau viongozi wao
 
ama hutengeneza mitazamo na hoja za kupinga matendo, kujitolea na maagizo ya viongozi wao. -Wanapenda kutekeleza maagizo wanayopewa uso kwa uso na sio yale ya jumuia -Wakiwa viongozi huweza kujikuta wakichukiwa na watu hasa pale watakapoendekeza tabia yao ya kutojali haja na matakwa ya wale wanaowaongoza.
 
3.SANGUINE -Wana uwezo wa kawaida kiakili (mara nyingine mdogo) -Ni wacheshi sana -Watu walio na maneno mengi na wasiopumzika kuongea -Wanajisikia raha sana pale wanapokuwa wakiongea na watu wengine wakiwasikiliza -Wanapenda kuanika mambo yao binafsi mbele ya wengine -Waigizaji wa kuchekesha wengi ni wakutoka katika
 
kundi hili -Wanapenda sana kujisifu na kujikweza -Wanapenda sana kusifiwa hata kwa mambo ambayo hayana uhalisia -Wanataka sana kuonekana mbele ya watu kwa kila jambo wanalolifanya. -Wanavipaji vingi vizuri lakini wanahitaji kusifiwa na kuhamasishwa ndipo huvionesha kwa
 
uhakika -Wana hisi za zima moto (i.e wanahamasika haraka na kusahau haraka. Ikitokea ajali huwa watu wa kwanza kujitokeza eneo la tukio na kuanza kutoa msaada; lakini akiondoka pale anasahau kila kitu na hata kama ametumwa akalete ambulance, anaweza kuanza kufanya shughuli zake nyingine) -Muda wote wako nadhifu (ni
 
wakereketwa wa masuala ya usafi na unadhifu) -Wana kiherehere sana. -Wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau -Ni vinyonga katika tabia zao (wana uwezo wa kuigiza tabia zisizo zao kiuhalisia na watu wasiowajua wasiwagundue kirahisi) -Wanashawishika haraka sana kupokea mambo mapya lakini ni rahisi
 
kuyaacha -Wasichana wa kundi hili si rahisi kurubuniwa kimapenzi kwa silaha ya ushawishi wa maneno, kwa sababu na wao wana maneno mengi -Ni kundi linaloathiriwa sana na love affairs (i.e wao ni multiple lovers-ni kawaida kumkuta sanguine akiwa na wapenzi zaidi ya mmoja: __inasemekana kutokana na maneno yao mengi na ufundi wa kuigiza hisia na tabia wavulana wanaume wa kundi hili huwanasa
 
wasichana kirahisi bila kutumia mtaji mkubwa.) -Wawapo kwenye jamii hukubalika sana hasa kutokana na ucheshi wao na ukarimu walio nao. -Wanapenda sana kuwasaidia watu ingawa ni kwa kujionesha -Ni wahamasishaji wakubwa na wenye ushawishi wenye kukubalika kirahisi -Ni kundi la wainjilisti wanaoongoza kwa kurudisha kondoo wengi kwa Bwana (wengi wana karama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…