Miongoni mwa matatizo ya kinywa yanayowasumbua watu wengi ni hali ya jino kutengeneza tundu kutokana na asidi au tindikali inayozalishwa na bacteria iliyomo kwenye vyakula vyenye sukari.
Kutoboka kwa meno mara nyingi husababishwa na utando wa asidi au tindikali izalishwayo na bacteria waliomo kwenye utando mlaini ambao hutoboa jino husika kuanzia kwenye tabaka la nje la jino na kuingia ndani.
Tatizo hili lisipozibwa mapema huenda likasababisha kung’olewa kwa jino husika ikiwa ni njia ya kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza endapo litaendelea kuwepo kwa mhusika.
Licha ya uimara wake, meno yanaoza. Ikumbukwe kutumia sukari mara kwa mara ni tishio kwa meno. Siyo vyakula vyenye sukari pekee hata vya wanga navyo ni hatari kwani vinaposagwa hutengeneza sukari ambayo nayo huchangia kuozesha meno. Hivyo basi kutumia vyakula na vinywaji vyenye sukari kwa wingi kati ya mlo mmoja na mwingine huongeza uwezekano wa kutoboka kwa meno kwani hushambuliwa muda wote na kukosa wasaa wa kupumzika. Hivyo ni muhimu kujiepusha na matumizi ya vyakula na vinywaji vya sukari kwa siku nzima ili kuimarisha meno.
Meno hutoboka wakati sukari iliyopo kwenye chakula inapotumiwa na bacteria walioko kwenye kinywa ambao baadaye hutengeneza tindikali inayoozesha meno na kuyatoboa. Kila mara unapokunywa au unapokula ama unapokunywa vitu vilivyo na sukari kwa wingi, tindikali hii huyashambulia meno na kuyatoboa.
Mara nyingi tindikali hii huweza kupunguzwa nguvu na madini ya chumvi yaliyomo kwenye mate ingawa na mashambulizi haya huweza kuchukua hata saa moja baada ya kula vitu vya sukari.
Zipo dalili za maradhi haya ambayo kwa kawaida yakiwa kwenye hatua za awali jino husika huweza kuwa na alama nyeupe kama ya chaki kwenye eneo linalotaka kutoboka.
Alama hii huonwa na daktari wa meno anapopiga mionzi jino husika. Weupe huu huwa hauna tatizo lolote kwa mhusika mpaka pale tundu litakapojitokeza ambalo nalo huchukua muda kabla halijaanza kuleta madhara yake.
Mgonjwa huanza kujisikia tofauti mara tu tundu lililoko kwenye jino linapofika sehemu ya kati ya jino. Jino huanza kuwa na maumivu hasa mhusika anapotumia ama vitu vya baridi au moto, au vya sukari au tindikali.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.