Sababu
Licha ya uimara wake, meno yanaoza. Ikumbukwe kutumia sukari mara kwa mara ni tishio kwa meno. Siyo vyakula vyenye sukari pekee hata vya wanga navyo ni hatari kwani vinaposagwa hutengeneza sukari ambayo nayo huchangia kuozesha meno. Hivyo basi kutumia vyakula na vinywaji vyenye sukari kwa wingi kati ya mlo mmoja na mwingine huongeza uwezekano wa kutoboka kwa meno kwani hushambuliwa muda wote na kukosa wasaa wa kupumzika. Hivyo ni muhimu kujiepusha na matumizi ya vyakula na vinywaji vya sukari kwa siku nzima ili kuimarisha meno.