Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwandishi wa kimarekani Annie Dillard aliwahi kuandika juu ya mwanamke mmoja mzee ambaye alisema: “Inaonekana tumewekwa tu hapa chini, na hakuna anayejua kwa nini.” Hakuna anayejua kwa nini? Hata katika sarufi mbaya, hisia kali za swali la siku nyingi – sisi ni akina nani? Tumekujaje hapa? Inatupasa tuishije? Makusudi yetu ni yapi? – linajitokeza katika maneno yake.
 
Ni maneno muhimu pia, kwa sababu hatuwezi kuishi maisha kamili nay a afya bila kujua chanzo na makusudi ya maisha hayo kama mtu anyefikiria kuwa ipad ni ubao tu wa kukatia figili na vitunguu jikoni, anaposhindwa kuitumia ipasavyo.
Wanadamu wamekuwa na nadharia na visa mbalimbali kuelezea chanzo chetu. Moja kati ya visa vya zamani kabisa kinasema, mungu mmoja alimwangusha mungu mwingine chini ambaye mwili wake ulikuwa dunia, na
 
kwamba kila wakati yule mungu aliyeshinda anapoitemea mate maiti ya adui yake aliyeshindwa, mwanadamu hutokea. Kwa upande mwingine, moja kati ya visa vipya kabisa kinafundisha kuwa hatupo kabisa, bali ni mifano ya kompyuta iliyotengenezwa na jamii yenye akili sana ya viumbe wasiokuwa wa dunia hii.
Katikati ya dhana hizi mbili, ikiwamo ya Alex Rosenberg anayeamini kuwa hakuna Mungu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…