Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Makusudi
Kinyume na dhana iliyoenea ya sayansi ya kisasa kwamba viumbe hai vya duniani vilitokea kwa bahati mbaya tu (dhana ambayo kwa kweli inatokana na falsafa na siyo sayansi), Maandiko yanaelezea kutokea kwa uhai kama tendo la moja kwa moja la Mwumbaji. Katika kitabu cha Mwanzo kila kitu kina makusudi – hakuna kilichotokea kwa bahati. Sisi si mkusanyiko wa kemikali
 
mbalimbali zilizopangiliwa kwa kudra. Fomula isemayo “Mungu akasema …iwe …ikawa hivyo” inaonekana kwa kujirudia kote katika maelezo ya uumbaji katika Mwanzo 1 na inaonesha azma ya makusudi ya moja kwa moja. Kila mstari unakanusha dhana ya kwamba kitu cho chote kilitokea bila mpango.
Makusudi kama hayo ni muhimu hasa inapokuja kwa
 
wanadamu. Badala ya kutamka tu tukatokea na kuwa hai, kama alivyofanya kwa viumbe hai vya duniani, Mungu alimfanya Adamu kwa udongo na kumpulizia uhai. “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai” (Mwanzo 2:7). Ni tendo la uhusiano wa karibu ambalo, pamoja na mambo mengine, limewafanya wanadamu wawe viumbe
 
Back
Top Bottom