Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

pekee walioumbwa kwa “mfano wa Mungu” (Mwanzo 1:27).
Uumbaji ulikamilika kwa kuwepo kwa wanadamu, kana kwamba yale yaliyotokea katika zile siku tano kabla yetu yalikuwa kwa ajili yetu tu. Baada ya kuumba wanadamu siku ya sita, Mungu alipumzika siku ya saba (Mwanzo 2:2), kwa kuwa kazi yake ilikuwa imekwisha: “Basi mbingu na nchi zikamalizika na jeshi lake lote” (aya ya 11).
 
Mwandishi mmoja wa kikristo, Ellen White aliandika kwamba “baada ya dunia na wanyama na mimea kuumbwa, aliumbwa mwanadamu, ambaye alikuwa kilele cha kazi ya Mwumbaji, na ambaye dunia ya kupendeza ilikuwa imefanywa ifae kwa ajili yake. Alipewa mamlaka juu ya vyote ambavyo jicho lingeweza kuviona.” Kinyume na dhana ya kifalsafa iliyoenea sasa, inayosema kwamba tulizuka tu, badala yake tulikusudiwa kuwepo hapa.
 
Kubadilisha Vipimo
Ingawa kitabu cha mwanzo kinafundisha kuwa Mungu aliiumba dunia maalum kwa ajili yetu, uvumbuzi wa hivi karibuni wa sayansi umefikisha utambuzi huo mpaka nje ya sayari yetu, mpaka kwenye sayari na nyote zingine. Unaonesha vipimo vingi visivyobadilika ambavyo havirushusu badiliko hata dogo kabisa bila kufanya kuwepo kwetu kusiwezekane.
Kwa mfano, uwiano katika kani ya sumaku-umeme na kani ya
 
uvutano ungebadilika kwa uwiano wa 1:10, wanadamu wasingekuwapo. Uwiano wa 1:10 inamaanisha nini? Mwanamahesabu John Lennox anaelezea: Lifunike bara la Amerika kwa sarafu na kuzipanga kwenda juuhadi mwezini (umbali wa kilometa 380,000), Kisha fanya hivyohivyo kwa mabara mengine bilioni moja yanayolingana na bara la Amerika. Ipake rangi nyekundu sarafu moja kasha uiweke mahali katika moja ya yale marundo.
 
Back
Top Bottom