Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ngozi ni muhimu kwa kila binadamu, hivyo kuhitaji kulindwa ili isidhurike na kuuathiri mwili licha ya kuwapo kwa zaidi ya magonjwa 6,000 yanayoweza kuushambulia.

Yapo magonjwa ya ngozi ambayo yakimpata mtu hupona haraka na kuiacha ikiwa katika hali yake ingawa mengine ni ya kudumu na yakitibiwa huchukua muda mrefu kupona, hivyo kumkosesha raha mgonjwa.
 
Dk Zeinabbas Ladha anasema ugonjwa huu ni miongoni mwa maradhi yanayotokea baada ya kinga za mwili kujishambulia (autoimmune reaction) na kuathiri seli za melanocytes (melanini), zinazotengeza rangi ya ngozi na kusababisha mabaka meupe katika baadhi ya maeneo ya mwili.
 
Anasema ugonjwa huu unaweza kutokea sehemu yoyote ya mwili na hausababishwi na bakteria wala vijidudu. Wagonjwa wengi, anasema wanaathirika zaidi katika maeneo yanayopigwa na jua kama vile usoni, mikononi, maeneo ya shingo na sehemu nyingine za mwili ingawa unaweza ukajitokeza sehemu yoyote.
 
Anasema sababu nyingine ya kupata ugonjwa wa vitiligo ni urithi kutoka miongoni mwa ndugu wa familia moja. Kwamba, mtu anayezaliwa kutoka kwenye familia ambayo imewahi kuwa na mtu mwenye ugonjwa huu naye anaweza akaugua.
 
0a8fea3a4e2b3ec29eb00275863ee39d.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom