Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tatizo la kutokuwa na uwezo wa kutoona vitu vilivyo mbali hutokea pale macho au jicho linapokuwa kubwa au sehemu ya jicho inayoruhusu mwanga wenye taswira kuingia ndani ya jicho; yaani cornea, kuwa
 
imekunjika kuliko kawaida hivyo kushindwa kuelekeza mwanga wenye taswira kutua kwenye eneo la nyuma la jicho linalohusika na kusafirisha kile kinachoonekana kwa ajili ya kutafsiriwa kwenye ubongo.
 
Hii husababisha retina kushindwa kupeleka taarifa zenye taswira kwenye ubongo na matokeo yake hushindwa kutafsiri taswira ambayo mtu anajaribu kuitazama. Matokeo yake ni wewe kushindwa kutambua unatazama nini.
 
Mpaka sasa sababu ya kwa nini watu wengine wanakuwa na macho makubwa, haijajulikana ila kuna hisia kuwa hali hii hutokana na vinasaba na ndiyo maana tatizo hili huoneakana zaidi kwenye familia zenye watu wenye tatizo hili.
 
Watu ambao kwenye familia kuna historia ya tatizo hili ndio wako hatarini kukumbwa na hali hii. Kama mzazi mmoja au wote wawili wana tatizo hili (na wanavaa miwani) basi kuna uwezekano wa karibu asilimia 95 kwa mmoja wa watoto kuwa na tatizo hilo pia.
 
Kwa watoto changamoto hii mara nyingi hutambulika tangu mtu mwenye tatizo hili akiwa mdogo kabisa kiumri au anaonekana akiwa amekunja uso au kufinya macho au anasogea karibu na runinga wakati anatazama au darasani mtoto anaonekana akisogea karibu na mwalimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…