Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ngozi ya matunda kama zabibu zinasaidia kulinda afya ya ngozi ya binadamu na kupunguza hatari ya mtu kupata ugonjwa wa saratani.
Ngozi na nyama za ndani za matunda kama machungwa ni chanzo kizuri cha nyuzi lishe, ambazo hupotea wakati wa kuchuja juisi.
 
Tikitimaji ni miongoni mwa matunda yanayopatikana kwa wingi nchini likiwa na virutubisho vingi vyenye faida kubwa ndani ya mwili wa mwanadamu.
Tunda hili ni chanzo cha protini, mafuta, nyuzinyuzi, wanga, calcium, phosphorus, potassium, magnesium, carotene, chuma, Vitamini A, B6 na C.
 
Licha ya kupatikana kwa bei nafuu, tunda hili huuzwa sehemu tofauti. Kwenye baadhi ya maeneo hata vipande vyake vinapatikana. Ingawa haishauriwi kula matunda yaliyomenywa, vipande vya tikitimaji huuzwa barabarani pia.
Hata hivyo, tikitimaji lina faida nyingi mwilini zinazotokana na wingi wa maji iliyonayo. Wataalamu wanaeleza kwamba asilimia 92 ya tunda hilo ni maji. Ni muhimu kwa afya na meno na fizi.
 
Linakinga uharibifu wa seli huku likisaidia uyeyushaji wa protini kuwa nishati na hurahisisha mzunguko wa damu mwilini.
Vilevile huondoa sumu mwilini na kwa mwanaume anayekula mbegu zake husaidia kuongeza nguvu za kiume. Huimarisha kinga za mwili na kuharakisha kupona kwa vidonda na majeraha.
Tikitimaji lina kiwango kikubwa cha Iycopene kuliko matunda au mboga zozote za majani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…