Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Matibabu

Tiba ya jino siyo kung’oa kama inavyoaminika. Ukweli ni kwamba kung'oa jino kutokana na sababu nyingi za kitabibu ambazo zinajitosheleza kwenye muktadha husika.

Kwenye tasnia ya tiba ya kinywa na meno, kung’oa jino lenye tatizo huwa ni hatua ya mwisho baada ya matibabu mengine kushindikana kutokana na sababu tofauti.
 
Sababu hizi zinaweza kuwa mgonjwa kushindwa kumudu gharama za kutibu jino lake pasipo kung’olewa au kutokua tayari kwenda hospitali mara kwa mara kwa ajili ya kuendelea na kukamilisha matibabu.

Nyingine ni mgonjwa husika kwenda hospitali wakati ana maumivu makali na huenda usiku wa siku hakula.

Baadhi ya wagonjwa huwa na aina ya matibabu wanayoyataka vichwani mwao. Hawa ni ngumu kuwabadilisha na kuwapa tiba mbadala kwa tatizo alilonalo.
 
Ili ufaidike na matibabu ya kitaalamu ni vizuri kuwa na utaratibu wa kufanya uchunguzi wa kinywa na meno mara kwa mara kabla ya mambo hayajaharibika. Kumuona daktari mapema kunaongeza uwezekano wa kuokoa meno yenye tatizo.

Mara nyingi kutibu jino lililotoboka ambalo halina maumivu ni nafuu Zaidi ukilinganisha na jino lenye maumivu.
 
Licha ya kung’oa, mgonjwa anaweza kuondokana na tatizo la jino lililotoboka endapo atazingatia ushauri wa daktari. Ushauri ni moja ya matibabu muhimu kwa watu wenye meno yaliyotoboka.

Kwa ushauri wa daktari mgonjwa atapata elimu ambayo wakati mwingine huweza kuwa msaada mkubwa kuliko kung’oa jino husika kama wengi wanavyofikiria. Elimu hii hutolewa kulingana na ukubwa wa athari zilizobainishwa na vipimo.
 
Dawa zinazotumika kuziba meno hutofautiana kulingana na mahali lilipo jino bovu hivyo gharama za dawa husika.

Kulijengea

Hapa ni kwa meno ambayo yameliwa na matundu na haiwezekani kuyaziba kikawaida. Matibabu haya huwa na hatua kadhaa. Pia yanaweza yasifahamike sana miongoni mwa watu wa kipato cha chini maana ni gharama.
 
Screenshot_2017-08-24-12-51-39.png
 
Back
Top Bottom