Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-08-24-12-53-22.png
 
Sababu

Zipo sababu nyingi zinazochangia meno kutoboka. Nyingi zinaepukika na mhusika kuwa na uhakika wa afya ya kinywa chake.

Mara nyingi meno yanayotoboka ni ya nyuma. Yanaitwa magego au masagego. Kwa umbile, yana mifereji ambayo ni rahisi kwa mabaki ya chakula kujishika. Yapo nyuma ukilinganisha na
 
meno mengine hivyo kuongeza ugumu wa kuyasafisha. Wengi hawafikishi mswaki maeneo ya nyuma ya kinywa.

Kutokana na hilo, tindikali huweza kujikusanya na kuyashambulia kwa urahisi zaidi kuliko meno ya mbele. Hii haimanishi ya mbele hayawezi kutoboka kwani watu ambao meno ya mbele yametoboka wakati ya nyuma ni mazima.
 
Vyakula na vinywaji

Baadhi ya vyakula na vinywaji huweza kujishika kwenye meno kwa muda mrefu. Hivi ni maziwa, ice cream, keki, na mkate hivyo kusababisha meno kutoboka kuliko vinywaji na vyakula ambavyo vinaweza kusafishika na kusafirishwa na mate kiurahisi.
 
Inashauriwa, si vizuri kumuacha mtoto kutwa nzima akiwa anakula ama anakunywa vitu vya sukari kwa faida ya afya ya kinywa chake.

Kutopiga mswaki

Ingawa inaripotiwa kuwa karibu kila mtu duniani anapiga mswaki, ukweli ni kwamba kuna upungufu kwenye upigaji huo miongoni mwetu. Watu wengi wana haraka kwenye kupiga mswaki hivyo kujikuta hawaufikishi sehemu zote za kinywa.
 
Kukosa floridi

Madini ya floridi huzuia kutoboka kwa meno na kusaidia kuliponya jino lililotoboka likiwa hatua za mwanzo.

Kutokana na faida yake madini haya huongezwa kwa makusudi kwenye maji ya kunywa kwa viwango stahiki.

Kutokana ukweli huo, unywaji wa maji ya kutosha kila siku, licha ya faida nyinginezo mwilini, huimarisha ubora wa meno.
 
Vilevile dawa za meno huwekwa madini hayo ili kuyaimarisha meno yetu. Ni muhimu kuhakikisha dawa ya meno unayotumia ina madini ya floridi.

Kinywa kikavu

Kinywa kikavu ni matokeo ya upungufu wa mate ambayo kiasili huzuia kutoboka kwa meno kwa kuondoa mabaki ya chakula na utando mlaini kwenye meno.
 
Vilevile kemikali zilizomo kwenye mate husaidia kupambana na tindikali izalishwayo na bakteria na kutoboa meno.

Ukavu wa kinywa huweza kuleta vitu vinavyoathiri meno kama vile baadhi ya dawa za kutibu magonjwa mbalimbali, magonjwa yanayoathiri matezi, matibabu ya mionzi ya saratani kichwani au shingoni.

Haya yote huongeza uwezekano wa kutoboka kwa meno kutokana na kupunguza uzalishaji wa mate ambayo ni kinga ya kwanza kuepuka kutoboka.
 
Kinadharia yes unatakiwa kutosheka na dada yetu uliyemtolea ng'ombe 30. Shida ya hii misambwanda haiishi na siku hizi ndo balaa. Juzi juzi posta mpya pale round about ya lipolisi lile wanapotaka kumuweka dayamondi pulatinamuz umepita msambwanda wa kufa mtu jamaa mmoja kageuza shingo mpaka akaiparamia nguzo ya umeme ngwee damu zikamtoka. Aliumia na damu kumtoka lakini jamaa wakamzomea tu.

Ukiwa na dada halafu unakata shingo kushangaa msambwanda ni kumkosea adabu. Anza kuwa unajikaza ikibidi fumba macho kabisa na usali kimoyo moyo. Ila ukiwa peke yako angalia hata macho yakudondoke ali mradi tu usianze kuulizia namba za simu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Siamini kama kuna mtu kamtolea ng'ombe 30 na bado anahangaika na misambwanda[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom