Licha ya kuwa mboga, bamia ina faida nyingi mwilini na kiuchumi. Hulimwa maeneo yenye joto, ukanda wa kitropiki ikiwamo maeneo makavu. Miongoni mwa faida zake mwilini ni kusaidia kuondosha vimelea vya sumu kwenye ngozi.
Vilevile, inasaidia kuimarisha afya ya nywele na kuongeza kinga ya mwili. Bamia ina kiasi kikubwa cha Vitamini C, K na folic acid ambayo husaidia mmeng'enyo wa chakula.
Wenye kisukari au majeraha wanashauriwa kula bamia kwa wingi kwani ina mchango katika kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu pamoja na kuimarisha mifupa na kuganda kwa damu.
Ina vitamini A ambayo inasaidia kutengeneza kinga dhidi ya maradhi na sumu ambazo zinaweza zikaingia mwilini. Mbali na hayo, bamia husaidia kulainisha choo na kuongeza hamu ya kula.
Inasaidia urahisi wa kumeza chakula na huboresha uwezo wa macho kuona. Kwa wenye uzito uliopitiliza na unene mkubwa, bamia hupunguza lehemu na kusaidia kukabiliana na magonjwa mbalimbali.
Ulaji wa bamia mara kwa mara kwa wanawake husaidia kuponya kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi mara kwa mara na hutibu pumu. Kwa wanaoitumia mara kwa mara, huongeza kinga ya mwili.
Ulaji wa bamia mara kwa mara kwa wanawake husaidia kuponya kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi mara kwa mara na hutibu pumu. Kwa wanaoitumia mara kwa mara, huongeza kinga ya mwili.
Bamia ina wingi wa virutubisho vinavyosaidia kuimarisha afya ya nywele. Kwa wanaofanya kazi za nguvu au mazoezi mazito, bamia inasaidia kupunguza uchovu wa mwili na msongo wa mawazo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.