Mazoezi mepesi ni pamoja na kukimbia mbio za taratibu, kutembea, kuogelea, kuruka Kamba, kufanya kazi ndogo ndogo, kuendesha baiskeli na kucheza mziki.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zimebaini kuwa mazoezi mepesi ndiyo yanayochangia watu kuishi maisha marefu zaidi. Hii ni hutokana na mazoezi haya kumuepusha mtu na magonjwa ya moyo, kisukari, shinikizo la damu na unene uliopitiliza.