Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-08-25-08-13-56.png
 
Mikate ya vegetables Unga wa ngano 1kg Nazi 1iliokunwa Pilipili manga nusu kjk Bizar nzima 1 kijk Mafuta nusu lita Samli kjk 1 Hamira kjk 1 B powder nusu kjk Kitunguu maji 1 Carrots 2 Hoho /pilipili boga2 Nyanya 2 Cotmir kjk 1 Chuja nazi yako kiasi ya glass moja weka katika blenda weka na carot hoho nyanya na kitunguu maji pamoj na cotmir saga pamoja hadi iwe lain iziwe na vipande pande Chukua unga safisha vizur weka katika bakuli add hamira b/powder chumvi kias bizar nzima pilipilimanga na samli changanya pamoja then mimina mchanganyiko wako wa tui anza kuchanganya kdg kdg huku ukikanda hadi upate donge moja lilikandika vyema. Wacha kwa mda wa dakika 10 lijikande kidg then kata madonge madg madg chukua kibao pakaa unga mbichi chini ili lisigande sukuma duara ila lisiwe jepes wastan tu then yapange katika trea uliopaka unga chini wacha yaumukee Weka pan yako jikon tia mafuta kiasi ya kutia mkate ukaeleea yakipata moto weka mkate wako achaa uive kieleea kama andazi ukiwa brown geuza upande wa pili nao choma hivyo hivyo ukiwa tyr epua weka katika tissue au gazet ujichje mafuta then fanya kama unauvunja yaani unaaukamata wote kwa pamoja katika kiganja chako kama chapat vile. Fanya ivo hadi yote imalizeee enjoy. Ni mikate mitamu sana utaifurahiaa na ni simple kuipika. Haichukui mda
 
Meat eggs ni tamu na ni rahisi kuipika jaribu uone utamu wakee very yummy. Nyama ya kusaga 1/2 Mayai 4 Cheese ya kipande Cream ya nestle kikopo 1 Meat masala Breadcrumbs kikombe 1 Thomu na tangawizi Na vitunguu maji Ukiwa na vitu hvi ndio unaweza kutengeneza hiioo
 
Cheese meat cake Nyama nusu kgs Mayai 9 Spices za nyama Cheese ilioparwa Carot 2 Hoho 2 Pilipili 1 Kitunguu maji1 Tangawizi kjk 1 Curry powder kjk 1 Cotmir bunch 1 Mafuta vijiko 3 Baking powder kjk 1 Ndimu 1 Chemsha nyama kwa viungo na tangawizi yako weka na ndimu acha iwive usitie maji yatatoka wenyewe ikiwa kavuu epua Ikipoa Chukua mayai saba weka katika blenda weka na nyama tia carot uliakata pamoja na hoho weka cotmir na pilipili saga pamoja mchanganyiko wako ukiwa tyr weka katika bakuli add kijiko kimoja cha baking powder na curry powder na pia uhakikishe mchanganyiko wako umekolea vizur viungo Chukua trea unayotaka kupikia weka mafuta ienee mote iweke jikoni katika oven ipate moto haswaaa Chukua mayai mawili yaliobaki yapige kwa chumvi na pilipili manga kidg yakiwa tyr mimina katika trea iliopata moto ufanye.kama omlet itandaze mote ikiwa imeshikana mimina mchanganyiko wako wa nyama iweke sawa halafu juu mimina cheese yako itandaze vizurrr choma hadi iwive ikiwa tyr kata vipande enjoy.
 
BAJHIA ZA SAMAKI Mahitaji: Samaki wa mnofu vipande 2, vikubwa Baking powder vijiko 2 vya chai Unga wa ngano kikombe 1 Kitunguu saumu kilichopondwa 1/2 kijiko cha chai Paprika 1/2 kijiko cha chai Sukari 1/2 kijiko cha chai Kitunguu maji 1 kilichokatwa katwa Majani ya kotmir yalokatwa katwa vijiko 2 vya chakula Hoho zilizokatwa katwa kijiko 1 cha chakula Yai 1 Maziwa 1/2 kikombe, utatia kdogo kidogo si lazima yatumike yote NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA: 1. Safisha samaki wako vizuri kisha mchemshe kidogo kwa chumvi, ndimu na pilipili manga. 2. Mnyambue samaki wako kupata chenga chenga unaweza mnyambua kwa mikono, blender au food processor. 3. Changanya unga, baking powder na spices katika bakuli, ukishachanganya vizuri and other tia mahitaji yalobaki isipokuwa maji/maziwa kisha changanya tena vizuri 4. Anza kutia maji taratibu ukiwa wachanganya hadi kupata uzito mzuri wa kuchoteka kwa kijiko au mkono usiwe maji maji sana. 5. Tia mafuta jikoni juu ya moto wa kiasi, yakipata moto chota mcha -
 
PANDAN CHIFFON CAKE VIPIMO MAHITAJI: A Majani ya Pandan 20 Tui la nazi 80-90ml Viini vya mayai 6 Sukari 25g Mafuta 70ml Unga Kikombe 100g MAHITAJI: B Ute wa yai 7 Sukari 100g Unga wa sembe 12g NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA 1. Kata majani ya Pandan kisha blend na tui la nazi hadi yawe laini, kisha chuja na upime Pandan Juice. 2. Chukua Viini vya mayai na sukari changanya koroga kwa pamoja hadi kuchanganyika. 3. Mimina Mafuta na Pandan Juice kwenye mchanyanyoko na endelea koronga. Kisha weka unga na uendelee kukoroga akikisha usiwe na madoge. 4. Washa jiko lako (Oven) kwa moto 325°F / 160°C 5. Saga ute wa yai kwa dakika chache kwa kutumia mashine ya kukorogea cake (cake mixer) mpaka povu kujaa. Tia unga wa sembe na sukari blend mpaka Cream ijae juu. 6. Tia kwa pamoja mchanganyiko wa Viini vya Mayai na wa Ute wa yai. Koroga mpaka uchanganyike kuwa rangi moja. 7. Pakaza Siagi kwenye sifuria ya kuchome cake na Mimina Unga, Sawazisha ukae sawa. 8. Ingiza sifuria ndani ya jiko (oven) kwa dakika 50 hadi 55 Keisha toa. 9. Wacha cake ipoe kisha tumia kisu kuachanisha sifuria na cake kutoka ndani ya sifuria na weka kwenye sahani tayari kwa kuliwa. Enjoy! -
 
CURRY PRAWNS* *MAHITAJI* Prawns kama nusu kilo (walio safishwa) Kitunguu 1 size ya kati (chopped ) Nyanya 2 kubwa (tomatoes chopped) Kitunguu saum (garlic) 1 tsp Tangawizi 1tsp Tui la nazi kikombe kasorobo 3/4 Bizari 1 tsp Curry powder (simba mbili) 2 tsp Pilipili ya unga 1 tsp Limau au ndim kipande Chumvi kiasi Mafuta ya kupikia 2 tblsp Tsp = kijiko kidogo cha chai Tblsp= kijiko cha kulia *MATAYARISHO* Weka mafuta kwenye frying pan iliyo na shimo au dish. Kaanga vitunguu kwa dakika 2 mpaka viwe laini visiwe vyekundu. Weka tangawizi, garlic, bizari na curry powder changanya kwa nusu dakika weka tomatoes. Wacha tomatoes ziive vizuri halafu weka pilipili ya unga na chumvi. Mix kwa dakika 1 weka tui la nazi acha lichemke lakini koroga usiachie mkono ili lisikatike. Kama dakika 3 halafu weka prawns kwenye tui wacha waive. Hawachukui muda kuiva. Wakisha kuiva weka ndimu onja kama kila kitu kiko sawa. Tayari kwa kuliwa na wali ama ugali au unachopenda. ENJOY.
 
Cake ya zabibu na nazi Cup 1 sukari Cup 1 mafuta Cup 1 na nusu unga Mayai 5 Ts 2 maziwa ya unga Nusu cup nazi kavu Vinegar ts 1 Maganda ya machungwa grate kdg Bp ts 1 Bicabonat ts 1 Maji nusu cup Zabibu kavu kdg Piga mafuta na sukari kisha tia mayai na vanila Baadae tia vitu vyote weka unga wako kwenye trey ya cake tupia zabibu juu choma - 1
 
mishkaki ya prons... prons....1 kg Vitunguu maji pilipili boga thom.. tangawizi uzile Pilipilimanga chumvi ndimu..kubwa moja mama sita source vijiko viwili vya kulia olive oil kijiko cha kulia chumvi pilipili ya kuwasha.. safisha prons mkia usiutoe ...weka spices zote ...wacha kama saa ili viungo vikolee... kata Vitunguu maji vipande vipande pamoja na Pilipili boga... chukua vijiti vya mishkaki anza kupanga prons kitunguu prons pilipili size unayotaka ... chukua tray weka jikoni ipake mafuta kidogo ...panga mishkaki yako kwenye trey kila mara uwe unageuza mpaka wawive.. shukran ....
 
NUNGHATAI 2 (eggless ) siagi 250gms samli 200gm sukari kikombe 1 4 cups unga vanila ya unga hiliki Rangi upendanyo. Kungu manga nusu kijiko cha chai b.powder kijiko cha chai 1 method changanya samli na siagi kwa mixture mashine iwe nyeupe na laini tia sukari endelea kusaga tia vanila na b.powder sanga uzuri tia kungumanga ikisha tia unga wako chanyanya kwa Mkono ukishachanyanyika uzuri fanya viduara vidogo gandambiza kwa kidole cha gumba tia rangi bake kwa 25 minutes Usifungue oven bada dakika hizo zima jiko ziwache nunghatai kwa oven for 15 minutes than zitowe tayari kwa kuliwa
 
CINNAMON ROLLS BUNS Mayai 2 Maji ya uvuguvugu ( warm water) kikombe kasorobo. Hamira Unga vikombe 3 na nusu Chumvi kidogo Sukari vijiko 2 tbs Samli/ siagi nusu kikombe. Sukari ya unga ya kutia juu Mdalasini wa unga Sukari ya brown kikombe 1 Siagi/ samli iliyoyayushwa Zabibu kavu ( raisin, sultanas) ( optional) Nuts unazopenda ( optional) NAMNA YA KUFANYA Chukua hamira tia kwenye maji ya uvuguvugu pamoja na mayai changanya weka kando. Chukua unga na ile sukari vijiko 2 tbs, chumvi na samli au siagi mimi nimetumia samli vegetable shortening changanya mpaka uone imekuwa chenga chenga hapo tia yale maji uliyochanganya na hamira na mayai ponda mpaka uchanganyike uweke uwache uumuke.baada saa moja hivi chukua
 
Back
Top Bottom