Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baridi ya bisi na gauti
Virutubisho vingi katika ndizi mbivu husaidia kupunguza vimbe kwa asili kama vile vimbe zitokanazo na magonjwa kama baridi ya bisi na gauti hivyo kwa kutumia ndizi inaweza kukusaidia kuondoa matatizo haya. Unashauriwa kutumia ndizi katika mlo wako wa kila siku kwani itakusaidia kuepuka matatizo haya yatokanayo na umri na mlo duni hivyo.
 
Kuongeza uzito
Pamoja na kupunguza uzito ndizi mbivu pia inaweza kutumika kuongeza uzito. Ndizi mbivu inapoliwa na maziwa humfanya mtu aongezeke uzito kwa haraka. Maziwa tutoa protini na ndizi hutoa sukari ambavyo kwa pamoja humfanya mtu anenepe. Ndizi mbivu pia humengenywa kwa urahisi sana hivyo mtu mdhaifu anaweza kula ndizi mbivu 5-6 kwa siku tofauti na milo mingine na zote zikamengenywa na kuingia mwilini. Hii hufanya mtu aongeze nguvu/nishati (calories) 500-600 ambazo huhitajika kuongeza uzito.
 
Kuvimbiwa
Ndizi mbivu inanyuzi ambazo husaidia chakula kutembea kwa urahisi katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula hivyo kukuepushia tatizo la kuvimbiwa. Pia nyuzi hizi husaidia kusukuma choo kwa wale wasiopata choo ambapo pia humfanya mtu aondokane na ile hali ya tumbo kunguruma au kujaa. Kwa kusukuma chakula na choo kwa urahisi kwenye mfumo wa chakula ndizi mbivu inaweza kumsaidia mtu aipatwe na saratani ya utumbo mkubwa na puru.
 
a20f94ea49f50cf33f11c93d6fb3bed1.jpg
 
Ulcers
Kwa miaka mingi ndizi imetumika kupunguza utindikali wa tumbo pale unapozidi. Ndizi pia huweza kudhibiti kiwango cha tindikali kinachoingia tumboni. Virutubisho vilivyopo kwenye ndizi hufanya chembe hai zilizopo kwenye ukuta wa tumbo kujenga ukingo ambao hulinda tumbo dhidi ya tindikali. Pia ndizi ina virutubisho ambavyo huzuia enzyme ya protease na kuondoa bakteria wanaohusishwa na kusababisha vidonda vya tumbo.
 
Magonjwa ya figo
Ndizi pia husaidia kuepuka matatizo mengi ya figo. Ndizi ina kiwango kikubwa cha potassium ambayo husaidia kusawazisha kiwango cha maji mwilini na kupunguzia figo mzigo na kuongeza kukojoa. Hili husaidia kuepuka limbikizo la sumu mwilini kwa kutoka kwa njia ya mkojo. Polyphenolic iliyopo kwenye ndizi husaidia figo kufanya kazi zake vizuri na kuepusha pia limbikizo sumu mwilini.
 
Afya ya macho
Ndizi mbivu kama ilivyo kwa matunda mengi ina antioxidant na carotenoids pamoja na mchanganyiko mzuri wa madini ambayo yanaweza kuimarisha afya yako ya macho. Matatizo mengi ya macho yameonyesha kupungua pale mtu anapotumia ndizi au matunda mimea lishe yenye virutubisho sawa mfano mlonge.
 
Kuulinda mfumo wa damu
Ndizi mbivu inamchango mkubwa katika kuhakikisha mfumo wa damu na hasa moyo unabaiki kuwa na afya kwa sababu mbali mbali. Ndizi mbivu inavirutubisho vinavyosaidia kutanua mishipa ya damu na pottasium hivyo husaidia kushusha pressure. Mishipa inapotanuka husaidia damu
 
kuzunguka vizuri na kufikisha hewa kwenye viungo vya mwili na kuboresha ufanisi wake. Damu inapozunguka vizuri husaidia kuondoa atherosclerosis (ile hali ya mishipa ya damu kukakamaa na kuwa midogo) na kupelekea stroke na mshtuko wa moyo. Nyuzi zilizopo kwenye ndizi husaidia kuondoa mafuta kwenye mishipa ya damu na hivyo kusaidia damu kuzunguka kwa urahisi.
 
Bawasili/Mgolo
Bawasili au mgolo ni ugonjwa ambao huhusisha kufanya choo kupita kwenye njia ya haja kubwa kwa ugumu hali ambayo inaweza kumfanya mtu kutokwa damu. Ndizi mbivu husaidia mtu kupata choo kwa urahisi hivyo kusaidia kuepuka kupata bawasili. Pia ndizi mbivu husaidia kuondoa vimbe na hivyo kusaidia kuondoa vimbe na maumivu ambayo huambatana na miwasho kwa wagonjwa wa bawasili.
 
Anemia
Ndizi mbivu zina kiwango kikubwa cha madini ya iron ambayo husaidia kutibu anemia kwani iron ni sehemu muhimu sana ya chembe nyekundu za damu. Anemia hutokana na upungufu wa chembe nyekundu za damu kutokana na mtu kukosa iron. Ndizi mbivu zina copper pia ambayo ni ya muhimu katika utengenezaji wa chembe nyekundu za damu
 
Back
Top Bottom