Siku za hivi karibuni jamii imeshuhudia wanafunzi wengi kutumia simu hizi kama njia mojawapo ya kurahisisha masomo yao ukizingatia watanzania hawana desturi ya kujisomea vitabu jambo linalosababisha kukosekana kwa umakini na ufanisi katika masomo yao.
Waandishi wa habari ambao pia wana mchango mkubwa katika utumiaji wa simu kutoa habari mbalimbali za jamii wanazungumziaje matumizi haya?
Licha ya kupata habari mbalimbali kupitia simu za kiganjani, watu wengi wamekuwa wakitumia simu hizo kwa kuweka picha na kuwasiliana na marafiki zao bila kujali muda wa kazi.
Takwimu zinaonyesha kuwa watanzania milioni thelathini kati ya milioni arobaini na nne wanamiliki simu za kiganjani, sawa na asilimia 68 lakini matumizi ya simu hizi kwa kiasi yanatofautiana na lengo kusudiwa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.