Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FAIDA ZA KUAMKA MAPEMA:
Watu Wengi huwa tunakuwa macho kwa muda mrefu wakati wa usiku badala ya kupumzika kwa kulala. Kuna sababu nyingi za mtu kuchelewa kulala zikiwemo kuendelea kufanya kazi aliyopanga kumaliza kwa siku hiyo,Kutolala usiku au kuchelewa kulala bila sababu ya msingi sio vizuri kiafya.
 
Utafiti unaonyesha watu wanaopata kupumzika vizuri na kuamka asubuhi na mapema huwa na furaha na afya njema. Vilevile utafiti wa hivi karibuni unaeleza kwamba watu ambao huchelewa kulala au ambao hawapumziki kwa muda wa kutosha hupata matatizo ya ''utendaji kazi mbaya wa moyo (bad cadiac functioning) yakiwemo mapigo mabaya ya moyo (heart rate) na shinikizo la damu (blood pressure).
 
Utafiti pia unaonyesha kwamba muda wa asubuhi (alfajiri) ni muda pekee mzuri wa kuweza kufanya mambo yako kwa umakini na ufanisi mkubwa kwa kuwa wakati huo ubongo unakuwa hauna msongo wa mawazo.
 
Kuamka asubuhi kumekuwa ni changamoto kwa watu wengi. Muda wa asubuhi wengi wamekuwa hawautumii vizuri. Kwa sababu ya kutoamka mapema, watu wengi wanakosa hata saa moja asubuhi ya kufanya mambo ambayo ni muhimu kwao.
 
Kuamka asubuhi na mapema, kunaweza kukusaidia kupata muda wa kufanya mambo ambayo kila siku umekuwa unasema hauna muda wa kuyafanya. Muda wa asubuhi unaweza ukautumia kwa mambo mengi mazuri. Muda wa asubuhi unaweza ukautumia kusoma kitabu, kuomba au kufanya tajuhudi (meditation), kupiga mazoezi na mengine mengi.
 
Utafiti unaonesha watu wengi waliofanikiwa wanaamka mapema. Wengi wanaamka si zaidi ya saa kumi na moja(11) asubuhi. Wanautumia muda wa asubuhi kufanya mazoezi na mambo mengine mazuri na muhimu kwao.
 
Kwa sababu ya umuhimu na faida za kuamka asubuhi, leo nakupa mbinu mbili muhimu za wewe kufanya ili uweze kuamka mapema asubuhi. Mbinu hizi nimekuwa nazitumia mimi mwenye na zimenisaidia kupata muda wa saa mbili mpaka tatu asubuhi wa kuandika na kufanya mambo mengine muhimu kwangu.
 
Kulala mapema
Watu wengi wanataka kuamka mapema na wakati wanachelewa kulala. Mwili wako unahitaji mapumziko ya kutosha. Kulala saa chache sana ni kuutesa mwili wako na utaamka umechoka sana. Lala mapema, ili uamke mapema. Unapolala, weka kila kitu pembeni na ulale, acha kujezea simu na kuangalia Tv na kujidanganya kwamba umelala
 
Mimi nimekuwa nahakikisha niko kitandani si zaidi ya saa nne usiku. Hii imekuwa inanifanya niamke mapema. Mara nyingi nimekuwa naamka saa kumi asubuhi na kupata muda wa kusali, kusoma, na kuandika makala kila siku. Hata wewe unaweza kama ukiamua
 
Mimi nimekuwa nahakikisha niko kitandani si zaidi ya saa nne usiku. Hii imekuwa inanifanya niamke mapema. Mara nyingi nimekuwa naamka saa kumi asubuhi na kupata muda wa kusali, kusoma, na kuandika makala kila siku. Hata wewe unaweza kama ukiamua
 
Kufanya mazoezi
Nimekuwa nafanya mazoezi angalau kila siku. Hii imenisaidia kuamka mapema nikiwa na nguvu na hamasa kila asubuhi. Siku ambazo sikupiga mazoezi, nimekuwa naamka nikiwa na nimechoka sana. Kupiga mazoezi kunasaidia kuufanya mwili wako uwe nguvu na kukupa hamasa ya kuamka mapema asubuhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…