Mwanamke mmoja aliamuwa kumwambia mume wake kuwa hajaona watu wabaya kama wazazi wake (wa mume wake) na jamaa zake (za mume wake)..
Mume akamuuliza kwanini wasema hivyo?
Mke akamjibu kwa sababu tukitajirika basi utawaona hapa kila saa, lakini tukifukarika basi hawaji kabisaa..
Mume akamjibu huo ndio ukarimu na tabia njema ya familia yangu, kwani nikitajirika wanajuwa nina uwezo wa kuwasaidia ndio maana wanakuja niwape msaada, lakini nikifukarika hawawezi kuja kwa sababu wanaona hali yangu na wanaona ni kunitia dhiki ndio maana hawajii, ni wakarimu na wenye kuelewa sana na nawapenda sana..