Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Majibu yako ya kishujaa kweli
Tangaza nafasi sasa litakalo kua na kichwa cha habari kua mke anahitajika
Sifa:
-Mwenye uwezo mzuri wa kulea na kutunza familia,pamoja na usafi
-Mwenye hofu ya Mungu na upendo tele
-Angalau awe na hata kadiploma
-Awe na uwezo wa kusimamia biashara vizuri
-Chura na urembo ni sifa ya ziada japo sijali sana.

Akae akijua anayetaka mke
-Ana mtoto wa kike mdogo
-Mfanya biashara na kiuchumi yupo vizuri[emoji41]
Hahahah Bob usijali, kesho tangazo litaruka hewani. Warembo wa kwenye huu uzi wakae tayari yaan mkao wa kula kbs. Yan tangazo litaruka mubashara kbs humu humu kwenye uzi wetu pendwa.
 
Mayai ni moja ya vyakula vichache ambavyo naweza kuviweka katika kundi la vyakula ‘bora zaidi’ kuliko vyote.

Mayai yamejaa viinilishe mhimu na vingi kati ya hivyo viinilishe havipatikani kirahisi katika vyakula vingi vya kisasa.

Zifuatazo ni faida 10 za kiafya zitokanazo na kula mayai kama zilivyothibitishwa katika tafiti nyingi duniani:
 
1. Mayai yana virutubisho vya kushangaza

Mayai ni moja ya vyakula vyenye virutubisho vizuri zaidi katika sayari dunia.

Yai moja zima lina viinilishe vyote vinavyohitajika kuibadili seli moja kuwa kifaranga cha kuku.

Yai moja kubwa lililochemshwa lina:

Vitamin A: 6%
Folate: 5%
Vitamin B5: 7%
 
Vitamin B12: 9%
Vitamin B2: 15%
Phosphorus: 9%
Selenium: 22% o

Mayai pia yana kiasi cha kutosha cha Vitamini D, Vitamini E, Vitamini K, Vitamini B6, kalsiamu na Zinki.

Yai moja pia linakuja na kalori au nishati 77, gramu 6 za protini na gramu 5 za mafuta yenye afya au mafuta safi kwa ajili ya mwili (healthy fats).

Mayai pia yana viinilishe vingine vidogo vidogo (trace nutrients) ambavyo ni mhimu kwa afya bora.
 
Hakika… mayai ni chakula ambacho ni karibu kimejikamilisha, mayai yana karibu kila aina ya kiinilishe mhimu tunachokihitaji kila siku.

2. Mayai huwa na kolesto nyingi lakini hayaathiri kolesto katika damu



Ni kweli kwamba mayai yana kolesto nyingi.

Ukweli ni kuwa, yai moja tu huwa na kolesto mg 212, ambayo ni zaidi ya nusu ya kiasi cha kolesto ambacho imependekezwa ule kwa siku ambacho ni mg 300.
 
Hata hivyo…ni mhimu kuelewa kuwa kolesto katika mlo huwa si lazima ipandishe kolesto ya kwenye damu.

Kwa kawaida Ini peke yake huzalisha kiasi kingi cha kolesto kila siku. Wakati tunapokuwa tumekula mayai zaidi, Ini lenyewe huzalisha kiasi kidogo zaidi cha kolesto ili kusawazisha hiyo tofauti.

Matokeo ya ulaji wa mayai hutofautiana toka kwa mtu mmoja hadi mwingine:
 
Asilimia 70 ya walaji wa mayai hawapati kabisa kuongezeka kwa kolesto .
. Asilimia 30 ya walaji wanaripotiwa kuwa wanatokewa kuongezeka kwa kolesto

3. Mayai huuongeza Msongamano wa juu wa lipoprotini kolesteroli (Kolesto nzuri)

Mayai huuongeza Msongamano wa juu wa lipoprotini kolesto ijulikanayo kwa kiingereza kama ‘High Density Lipoprotein’ (HDL). Ambayo hujulikana kama ni kolesto nzuri, maana kuna kolesto nzuri na kolesto mbaya.
 
Watu wenye msongamano wa juu wa lipoprotini kolesto kwa kawaida huwa na uwezekano mdogo wa kupatwa na maradhi kama ugonjwa wa moyo, kiharusi (stroke) na matatizo mengine mengi ya kiafya.

Kula mayai ni njia nzuri ya kuongeza msongamano wa juu wa lipoprotini kolesto.

Katika moja ya majaribio; kula mayai 2 kwa siku kwa wiki 6 kuliwezesha kuongezeka asilimia 10 ya msongamano wa juu wa lipoprotini kolesto

4. Mayai yana kiinilishe mhimu sana kiitwacho ‘Choline’
 
Back
Top Bottom