Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

PAPAI: Ni tunda sahihi kabisa katika kukupa ngozi yenye mafuta, kurudishia au kuziba sehemu zilizoumia na kunyofoka katika ngozi yako. Papai pia hunga'arisha rangi ya ngozi yako, yote haya hufanyika na enzyme inayotokana papai ambayo huitwa papain. Endapo kama unataka kutumia papai katika ngozi yako ya uso, basi chukua asali changanya na papai lililo iva na paka usoni kwako kwa dakika 10 kisha safisha, kisha utaona kitakachotokea katika uso wako, utaonekana kama ngozi ya mtoto wa siku mbili.
 
CHUNGWA: Hili ni chungwa maarufu sana linalosaidia kurudishia ngozi iliyodhurika na kuupa uhalisia wa ngozi yako. Jinsi ya kutumia ni rahisi sana, chukua juisi ya chungwa ya baridi kisha paka usoni, acha kwa dakika 10 kisha osha utaona matokeo yake.
 
Fahamu faida za matunda haya kwa ubora wa afya yako.
Kuna faida nyingi za kula matunda licha ya kupenda ladha tamu za matunda tunayokula. Matunda yana virutubisho vingi ikiwa vitamin A na C hupatikana kwenye matunda mengi ukilinganisha na virutubisho vingine vilivyopo kwenye matunda mengine.
 
Matunda husaidia kupunguza matatizo ya moyo( heart diseases ), stroke ( kiharusi ), shinikizo la damu ( blood pressure ), cholesterol, aina mbalimbali za saratani (cancer ), matatizo ya uwezo wa macho kuona na mengine mengi.
Matunda yote yana manufaa kwa miili yetu lakini napenda ujue haya machache kuhusu faida za apple, parachichi, ndizi, zabibu, embe, chungwa, papai na nanasi. Matunda haya niliyoyataja huwa tumezoea kuyala lakini
 
naamini wengi wetu hatujui sana kuhusu ni vitu gani tunanufaika kutokana na kula matunda haya.
Zijue faida za matunda.....
APPLE.
-Hupunguza uwezekano wa kupata kisukari ( diabetes ) na pumu (asthma )
-Husaidia kinywa kutokuwa na harufu mbaya ( natural mouth fresher ) vilevile apple husafisha meno kila unapotafuna.
 
naamini wengi wetu hatujui sana kuhusu ni vitu gani tunanufaika kutokana na kula matunda haya.
Zijue faida za matunda.....
APPLE.
-Hupunguza uwezekano wa kupata kisukari ( diabetes ) na pumu (asthma )
-Husaidia kinywa kutokuwa na harufu mbaya ( natural mouth fresher ) vilevile apple husafisha meno kila unapotafuna.
 
Je Unajua? Harufu nzuri ya apple hupatikana kwenye maganda/ngozi yake, hivyo ni vyema ukalitafuna pasipo kulimenya kwani vitamin nyingi pia hupatikana kwenye maganda/ngozi ya juu.
PARACHICHI.
-Ni chanzo cha vitamin E.
 
Hupunguza kiwango cha cholesterol mwilini.
-Kwa afya njema ya moyo wako, kwenye sandwich au mkate tumia parachichi badala ya siagi.
Je Unajua? Watoto hupenda sana kula parachichi kwasababu ni laini na pia mafuta ya parachichi husaidia katika kukuwa kwa mtoto na kuwa mwenye afya bora.
 
NDIZI.
-Ni chanzo cha vitamin B6 na madini ya potassium.
-Licha ya kuwa na ladha nzuri, ndizi zina madini mengi ya potassium ukilinganisha na matunda mengine ambayo husaidia kupunguza ongezeko la shinikizo la damu ( blood pressure ).
Je Unajua? Watu wenye aleji na material ya mpira( rubber latex ) wanaweza pia kuathirika kwa aleji ya ndizi kwakuwa mpira na ndizi vyote zina aina moja ya protini.
 
ZABIBU.
-Ni chanzo cha madini ya manganese.
-Hupunguza uwezekano wa kupata maradhi ya moyo kwa kusaidia kushusha kiwango cha shinikizo la damu ( blood pressure )
-Huepusha magonjwa ya aina mbalimbali za saratani kwa kuzuia usambaaji wa seli za saratani ya titi ( breast cancer ), tumbo ( stomach cancer ) na utumbo ( colon cancer ).
Je Unajua? Unaweza gandisha zabibu za kijani na nyekundu na ukazitumia kama barafu ( ice cubes ) kwenye kinywaji chako upendacho.
 
EMBE.
-Ni chanzo cha vitamin A na E.
-Vitamin A iliyopo kwenye embe husaidia kuboresha macho yako kwa kukuwezesha uweze kuona vizuri. Pia husaidia kupunguza uwezekano wa upofu kwa wazee kwa kuimarisha macho yao.
Je Unajua? Embe ni tamu sana likiwa limeiva lakini pia likiwa bichi unaweza kutumia embe kutengenezea kachumbari, achali, chutney na salad.
 
CHUNGWA.
-Ni chanzo cha vitamin C na madini ya potassium.
-Chungwa lina vitamin inayojulikana kama ‘’folate’’ ( B-Group Vitamin ) ambayo husaidia katika kujengeka kwa ubongo wa mtoto kwa mama mjamzito.
-Chungwa lina kemikali zinazojulikana kama ‘’hesperidin’’ ambazo hupunguza kiwango cha cholesterol kwenye damu.
Je Unajua? Sehemu nyeupe ya chungwa ( gome lililo ndani ya chungwa ) lina thamani ya vitamin karibia sawa na nyama ya chungwa hivyo ni vyema kula chungwa lote baada ya kumenya maganda yake.
 
PAPAI.
-Ni chanzo cha vitamin A na C.
-Papai lina enzyme ijulikanayo kama ‘’papain’’ ambayo husaidia katika kusaga au mmeng’enyeko wa chakula.
-Pia vitamin A iliyopo kwanye papai husaidia husaidia kuboresha afya ya ngozi yako.
Je Unajua? Mbegu nyeusi za papai zinaweza kuliwa japo kuwa ni chungu lakini unaweza kuzisaga na salad kwa kutumia blender badala ya pili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…