Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Licha kumilikiwa na Marekani, kiko maili 8000 kutoka Marekani na inachukua takriban saa 19 kusafiri kwa ndege kutoka mji wa New York.
Wamarekani wanaweza kuelekea katika kisiwa hicho bila kutumia pasipoti.
Kila mtu aliyezaliwa kisiwani Guam ni Mmarekani lakini hawezi kumpigia kura rais.
 
Tangu mwisho wa vita vya dunia , watu wawili waliokuwa wakiishi katika kisiwa hicho walipewa uraia lakini hawawezi kumpigia kura rais wa Marekani. Wana mwakilishi mmoja wa serikali laki yeye hana uwezo wowote kuhusu utengenezaji wa sera.
Guam ni kambi muhimu ya kijeshi
 
Robo ya kisiwa hicho kinamilikiwa na jeshi la Marekani na kinatumiwa kama kambi ya wanamaji na wanaanga
Pia inakadiriwa kwamba karibia asilimia 10 ya watu wa Guam wenye idadi ya 160,000 ni ya wanajeshi.
Raia wa Guam wanajulikana kama Chamorro.
 
Chamorro ni jina la jumla linalopewa watu wanaoshi katika kisiwa cha Guam na watu wanaoshi katika visiwa vya Micronesia katika bahari ya Pacific.
Utamaduni wao unafanana na ule wa Uhispania zaidi ya Umarekani kwa sababu Uhispania ilidhibiti kisiwa hicho kwa takriban miaka 300 hadi 1898.
Watu katika eneo hilo hawatozwi kodi
 
Watalii kutoka Taiwan , Korea Kusini na Japan huchukua saa nne kusafiri hadi katika kisiwa hicho kwa likizo ya kupata jua mbali na kununua vitu ambavyo havilipishwi kodi.
Maduka yote makubwa huuza bidhaa za mitindo na mengi hufunguliwa kwa saa 24 kwa siku.
Ricardo Blas Jr. ndio mtu maarufu zaidi katika kisiwa cha Guam
 
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 30 ni mchezaji wa judo ambaye alishiriki judo katika michezo ya Olimpiki ya 2008 na 2012 na alibeba bendera ya Guam katika mashindano yote lakini akashindwa kupata medali licha ya kuwa mchezaji judo mwenye uzani mzito zaidi wa kilo 21
 
Back
Top Bottom