Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unangalia Simu Yako Kila Saa, Mara Nyingine Bila Sababu
Kuangalia simu ni jambo la kawaida lakini kama unajikuta unatabia ya kuangalia simu yako kilamara hata kama huna jambo lolote la msingi unalo fanya basi, moja kwa moja unaweza kuanza kutambua kuwa unalo tatizo la kupenda simu kupita kiasi.
 
Unashika Simu Yako Mara tu Unapo Amka na Mara Unapo Lala
Hapa naomba tuelewane kwani si maanishi kushika simu pale unapokua na ratiba nyingine usiku hapana, hapa na maanisha pale unapokua kitandani unapo tafuta usingizi nilazima ushike simu yako au pale unapo amka asubuhi hata kabla ya chochote unashika simu yako kwanza. Kama una dalili hii kwa muda sasa ni vyema uka fikiria kuiacha kwani inawezekana una tatizo la kupenda simu hupita kiasi.
 
Kama umefikia hatua unahisi kama simu yako inaita na wakati haiti basi jua kuwa inawezekana unalo tatizo hili na mbaya zaidi ni pale unapo fikia hatua ya kuhisi hivyo mara zaidi ya moja kwa siku na mara nyingi zaidi kwa wiki.
 
Ukitembea Unashika Simu Mkononi Badala ya Kuweka Mfukoni
Mara nyingi tukiwa kwenye mwendo hatuwezi kutumia vizuri simu zetu, lakini kama unaona mara nyingi unatatizo la kushika simu yako mkononi huku ukitembea hata kama huitumi basi kuna uwezekano una tatizo la kupenda simu kupitiliza.
 
Unakimbilia Kushika Simu Yako Unapopata Tukio la Aibu
Kupata aibu ni sehemu ya maisha ya kawaida lakini kama unajikuta kwa mara nyingi pale unapo pata aibu flani unakimbilia kushika simu yako basi jua kabisa uwezekano upo kuwa una tatizo la kupenda simu kupita kiasi.
 
Unatumia Simu Yako Hata Unapo Kuwa Unangalia TV
Hii sio sawa na mtu kuwa amechoshwa na kitu flani ukiwa mahali fulani, bali hii ni pale unapokuwa nyumbani unakuta unao uwezo wa kuzima au kubadilisha channel kwenye TV yako lakini unajikuta unatumia simu yako huku unangalia TV. Kama kwa namna yoyote unayo tabia hii uwezekano wa kupenda simu kupita kiasi ni mkubwa.
 
Unakuwa Unafanya Kazi za Muhimu Kupitia Simu
Hapa nazungumzia, kwa mfano mara nyingi unajikuta unajisikia vizuri kutuma barua pepe kwenye simu zaidi ya kutumia kompyuta hata kama unayo na hata kama barua pepe hiyo ni ndefu na inahitaji umakini. Kama unatabia hii ni vyema kuwa mwangalifu.
 
Unakuwa Unafanya Kazi za Muhimu Kupitia Simu
Hapa nazungumzia, kwa mfano mara nyingi unajikuta unajisikia vizuri kutuma barua pepe kwenye simu zaidi ya kutumia kompyuta hata kama unayo na hata kama barua pepe hiyo ni ndefu na inahitaji umakini. Kama unatabia hii ni vyema kuwa mwangalifu.
 
Muda Unaenda Sana Ukitumia Simu Yako
Hapa na maana kuwa mara nyingi unajikuta unatumia simu yako mpaka unashtuka hivi kumbe muda flani umefika..!, kama unayo tabia hii na imetokea mara nyingi sana basi unalo tatizo hili.
 
Muda Unaenda Sana Ukitumia Simu Yako
Hapa na maana kuwa mara nyingi unajikuta unatumia simu yako mpaka unashtuka hivi kumbe muda flani umefika..!, kama unayo tabia hii na imetokea mara nyingi sana basi unalo tatizo hili.
 
Simu Kwako ni Kitu cha Muhimu Kuliko Kitu Chochote
Kama unayo tabia ya kujali simu yako kuliko kitu chochote kile basi inawezekana kabisa unalo tatizo hili la kupenda simu kupita kiasi.

Na hizo ndio baadhi tu ya dalili ambazo leo nimeweza kukuchambulia ili kuweza kujua kuwa una tatizo la kupenda simu kupita kiasi, Tatizo hili linaweza kuisha kwa kujizoesha mambo mbalimbali kama kucheza mpira mazoezi au vitu vingine kama hivyo.
 
Ni vyema uka amua kumuona mshauri kama utashindwa kabisa kuacha tabia hii kwani, hili ni tatizo sugu kama yalivyo matatizo mengine ambayo ni ngumu kuyaAcha, kumbuka kupenda simu kupita kiasi kunaweza kusababishia matatizo mbalimbali kama ya Afya, matatizo ya kifamilia, kimahusiano na mambo mengine kama hayo.
 
Back
Top Bottom