Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station

"Naitwa John nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki 7, ATM Card na kikaratasi chenye PIN ya ATM Card na kijimkufu cha dhahabu kinene hivi…"

Mtangazaji akasema:- Akhasante sana John, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama ana kusikiliza akutafute kwa No. Gani!?

John: Hapana, mi nilikuwa namshukuru tu maana amenitoa kwenye matatizo na ninapenda kumuombea Dedication wimbo wa Snura "MAJANGA" umfikie popote pale alipo…!!!
 
jamaa Wawili Walifika Stesheni, wakakuta Treni ndo kwanza inaondoka. Wakaanza Kuikimbiza. Mmoja akafanikiwa kupanda akaondoka…

Yule aliyebaki akaanza kucheka sanaa mpaka machozi yakamtoka. Watu wakamuullza, unacheka nini sasa wakati umeachwa? Akawajibu: "kinachonichekesha, yule aliyepanda alikuwa ananisindikiza.
 
Uzuri wa ngozi sio rangi tu bali ni muonekano wa ngozi yenyewe kwamba ina afya na mng'ao unaoashiria afya njema.

Leo tushirikishane jinsi ya kufanya facial treatment kwa kutumia vitu vya jikoni kama kiini cha yai,machicha ya nazi,tango na limao.Treatment hii inaweza kufanyika Mara moja kwa wiki au kila baada ya wiki mbili, unaweza kufanya hata mara moja kwa mwezi ukipata nafasi kama unakuwa busy sana lkn matokeo mazuri utayashuhudia.
 
Jinsi ya kufanya

Andaa maji masafi yenye joto kiasi unachomudu ktk ngozi yako, osha uso wako kwa hayo maji safi .
Kama una ngozi kavu au ya kati chukua kipande cha tango kidogo na upake yale maji yake usoni, kwa wenye ngozi ya mafuta unaweza kutumia kipande cha limao kwa kupaka maji yake. Chukua pamba au kitambaa laini na futa maji ya matunda usoni kwa mtindo wa kusafisha taratibu usoni.
 
Chukua machicha ya nazi na Anza kuusugua uso na shingoni taratibu Mpaka uridhike uso wote umepitiwa na machicha yako hasa unapoona unang'aa kwa mafuta kidogo yaliyotoka kwenye nazi. Kisha pukuta yale machicha ubaki na uso unaong'aa bila vitu vyeupe yaani machicha.
 
Chukua kiini cha yai inapendeza ukitumia la kienyeji, au la kisasa lenye kiini cha njano iliyokolea angalau. Ili kiini kisijichanganye na ute wakati wa kupasua ,ligonge yai upande mmoja sio katikati na limimine ktk chombo mithili ya sahani ambayo unaona kiini katikati kisha unakichota na kuweka kando. Paka ule uji mzito wa njano wa kiini uso mzima bila kusahau shingoni na nyuma ya masikio na ngozi ya masikio.
 
Ngozi yenye mafuta kwa kawaida huwa inang'ara, nene na yenye rangi iliyotitia. Mara nyingi ngozi yenye mafuta mengi sana huwa na chunusi nyingi na vipelepele na mara nyingine huwa na chunusi zenye vichwa vyeusi. Katika aina hizi za ngozi mafuta hutokana na tezi za sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango kinachotakiwa. Mafuta hayo husambaa katika ngozi na kuifanya iwe na mafuta mafuta.
 
Back
Top Bottom