Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

d57d7427b19309da8e551f81d829f2e5.jpg
 
kumekua na kesi mbalimbali za vifo sababu ya watu kumeza dawa kisha kujisahau na kunywa pombe.hii ni changamoto kubwa sana kwenye sekta ya afya..kawaida dawa yeyote anayopewa binadamu kutibu kitu fulani ni sumu na ikichanganywa na baadhi ya kemikali kama pombe huweza kudhuru na kuua kabisa hivyo leo naenda kuzungumzia dawa kadhaa amabazo ukiona umezimeza usiguse pombe kabisa.
 
dawa za kutibu bacteria[antibiotics];
hizi ni dawa ambazo hutumika mara kwa mara kwenye jamii kutibu magonjwa mbalimbali kama vidonda, kikohozi, kifua kikuu, madonda ya tumbo na kadhalika.matumizi ya dawa hizi na pombe huweza kuua. mfano fragile. isoniazid,grisiofulvin. lakini pia na baadhi ya dawa za malaria kama quinine na dawa za ya mseto ya malaria ni hatari zikitumika na pombe.
 
dawa za kuzuia damu kuganda[ant cougulant];
kuna dawa amabazo hupewa kwa wajawazito mara nyingi kulainisha damu ili isigande....sasa matumizi ya pombe hufanya dawa hizi kushindwa kufanya kazi na kusabisha damu kuganda hivyo kuziba mishipa ya damu ana kuleta kifo..mfano warfin
 
dawa ya kupunguza mgandamizo wa mawazo[ant depressant];
pombe huingilia kazi ya dawa izi na kufanya dawa hizo ziongezeke kwenye damu kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyopangwa. hii humfanya mgonjwa alegee sana mfano amitriptyline.
 
dawa za kutibu kisukari[ant diabetic];
dawa za kisukari hutengenezwa kwa ajili ya kushusha kiasi kikubwa cha sukari mwilini, sasa matumizi ya dawa hizi na pombe husababisha hali moja kitaalamu kama lactic acidosis... dalili ya hali hii ni maumivu ya misuli,tumbo kuuma na kusikia usingizi.hali hii isipodhibitiwa hospitali huua.mfano metformin vidonge.
 
dawa za mafua na aleji;[ant histamine]
hizi dawa hutolewa kutibu mafua, miwasho ya ngozi na kikohozi lakini dawa hizi pia husababisha usingizi na uchovu kila zikitumika.pombe huongeza uzingizi huu na uchovu mara duvu na kufanya mtu ashindwe kazi. mfano promethazine maarufu kama fenigani na chlropherinamine maleate maarufu kama piriton.
 
dawa za magonjwa ya akili;
dawa za akili kama chlopromazine hutolewa kwa wagonjwa wa akili kupunguza dalili a magonjwa haya kwa kuwapa usingizi...sasa matumizi ya pombe huongeza usingizi huu maradufu na kuwafanya washindwe kupumua hivyo huweza kuleta kifo.
 
Back
Top Bottom