Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

dawa za kutibu madonda ya tumbo;
mara nyingi madonda hutibiwi na mchahnganyiko wa dawa tatu kitaalamu kama triple therapy, sasa moja ya mchanganyiko huo kama cimetidine, metronidazole,scenidazole au tinidazole hazitakiwi kuchanganywa na pombe kabisa sababu ya madhara ambayo zimeonyesha.
 
dawa za moyo;
hichi ni kikundi kikubwa cha dawa ambacho hutumika kutibu matatizo ya moyo. matumizi ya dawa hizi wakati mwingine huingilia mfumo wa kazi wa mwili na kusababisha kizunguzungu na kuanguka wakati wa kusimama mfano methyldopa, hydralazine na isosorbine mononitrate na dinitrate lakini pia matumizi ya pombe hupunguza uwezo wa dawa ya presha kitaalamu kama propanalol na kuzuia uwezo wake wa kufanya kazi.
 
003e38d8146c94eb2670248df30e8e00.jpg
 
dawa za maumivu makali;
kuna dawa za maumivu kali sana ambazo hutolewa kwa wagonjwa wenye maumivu makali kama ya kansa, uzazi na maumivu ya ajali. pombe huongeza wingi wa dawa hizi kwenye mfumo wa damu na kusababisha overdose yaani dawa kua nyingi mwilini pale inapomezwa na pombe hata kama ulimeza dozo sahihi.mfano morphine,pethidine, codeine,meperidine...hali hii huleta kifo mara nyingi kwani wasanii wakubwa kama michael jackson na prince waliuawa na hali hizi.
 
dawa za usingizi;
dawa za usingizi kama valium hutumika kwa wagonjwa wenye kushindwa kupata usingizi na wakati mwingine kwenye chumba cha upasuaji. dawa hizi huleta usingizi mkali...matumizi ya dawa hizi na pombe huongeza usingizi huu, hupunguza mapigo ya moyo, hupunguza uwezo wa kupumua, kupoteza fahamu na kifo lakini pia dawa za kifafa kama phenytoin hupunguzwa uwezo wake na pombe na kushindwa kuzuia uwezo wake wa kuzuia degedege za kifafa.
 
Back
Top Bottom