Inategemea na ukubwa wa athari. Kama mpangilio haujawa mkubwa sana mpangilio mbaya huweza kujirekebisha wenyewe iwapo mtoto ataacha kunyonya kidole. Kwa wale wanaopitiliza wanahitaji huduma za mtaalamu wa meno (orthodontist) kufanya marekebisho.
Inategemea na ukubwa wa athari. Kama mpangilio haujawa mkubwa sana mpangilio mbaya huweza kujirekebisha wenyewe iwapo mtoto ataacha kunyonya kidole. Kwa wale wanaopitiliza wanahitaji huduma za mtaalamu wa meno (orthodontist) kufanya marekebisho.
Inashauriwa kutomkataza mtoto kunyonya kidole akiwa chini ya miaka minne au mitano isipokuwa kama kuna tatizo linalojitokeza au mtoto akianza ghafla kufanya, hivyo baada ya miezi kumi tangu azaliwe na ikiambatana na kuvuta nywele.
Ili kupunguza uwezekano huo, mama anayenyonyesha anapaswa kula vyakula vyenye lishe kamili vitakavyosaidia mwili kutengeneza maziwa ya kutosha kumnyonyesha na kumshibisha mtoto kila wakati, hivyo kumuepusha kunyonya kidole.
Kwa mtoto anayenyonya, wazazi au walezi wanapaswa kumueleza kwa upole wakitumia lugha laini ikibidi kumuahidi zawadi nzuri ili akubali kuacha kunyonya kidole.
Kumuanzisha shule ni njia nyingine inayoweza kumsaidia mtoto kuacha kunyonya kidole. Shule kutamfanya aone aibu hasa atakapokuwa anataniwa na wenzake anaosoma na kucheza nao.
Njia mbadala pia zinaweza zikatumika. Hizi zitamsaidia kuacha mapema zaidi. Kupaka pilipili vidole vyake ili akinyonya awashwe na ukali wa atakaokutana nao itamfanya asirudie tena kufanya hivyo ingawa kutakuwa na jukumu la kubembeleza atakapokuwa analia baada ya kunyonya kidole
Kushiriki michezo inayoshughulisha mikono kwa muda mwingi ni njia nyingine ya kufanikisha suala hili. Unaweza ukampa midoli au wanasesere, au acheze na wenzake ili mradi viganja vyake viwe na shughuli ya kufanya na kumnyima nafasi ya kunyonya kidole.
Pia, unaweza kumnunulia nyonyo za plastiki ili umpe anyonye badala ya kidole. Hii itamfanya asipate muda wa kuzoea kunyonya kidole na hatotumia muda mwingi kunyonya nyonyo hizo.