Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Watu wasiosafisha vyombo vya chakula kwa maji salama au wanaotumia vyombo vilivyooshwa vikiwa bado vina majimaji wanajiweka kwenye hatari ya kupata maambukizi haya. Vyombo vinatakiwa vifutwe kwa kitambaa safi mara tu baada ya kusafishwa.
Chakula kitakachochelewa kuliwa kinapaswa kufunikwa ili kuepusha inzi kutua kabla hakijatumika na kuacha bakteria wanaoneza maradhi haya.
 
Watu wengine wanaopaswa kuwa makini zaidi ni wale wasionawa mikono baada ya kutoka kujisaidia au wanaobanwa na haja sehemu ambazo hazina huduma ya choo na wanaotumia vyoo vya umma au wasafiri.
Dk Katoto Nestory kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) anasema wanafunzi na watu wanaokula kwenye vibanda vya mamalishe ambavyo havizingatii usafi wa vyombo vya chakula ni waathirika wakubwa wa ugonjwa wa amoeba.
 
Dalili
Mtu mwenye ugonjwa wa amoeba hukumbwa na dalili nyingi kama tumbo kujaa gesi, uchovu, kupoteza uzito, maumivu makali ya kichwa, kichefuchefu na kutapika.
Dalili nyingine ni homa, kutonusa vizuri harufu ya chakula na kutohisi ladha. Wapo wagonjwa wanaopata maumivu makali ya tumbo, kunyonga na kupata choo kisichoisha (tenesmas).
 
Mgonjwa hupata choo kilichochanganyika na kamasi na endapo ataenda chooni mara nyingi huishiwa nguvu, wakati mwingine hushindwa kutembea.
Dk Katoto anasema mara nyingi watu huwa na bakteria wanaosababisha ugonjwa wa amoeba bila kuhisi dalili zake na kutahadharisha kwamba hata kuumwa tumbo au kuhara pekee hakutoshi kuthibitisha maradhi haya bali kupima choo ndio njia pekee ya kuthibitisha.
 
Kuna watu ambao hawaumwi lakini wanao bakteria wanaosababisha ugonjwa wa amoeba miilini mwao. Hawa ndio mara nyingi husababisha kuenea kwa ugonjwa huu kwani ingawa hawapati madhara huweza kuambukiza watu wengi,” anasema Dk Katoto
Madhara
Dk Katoto anasema ugonjwa huu unatakiwa kutibiwa mara tu mgonjwa anapogundulika na maambukizi ili kumuepusha na madhara mengi yanayoweza kujitokeza.
 
Endapo mgonjwa hatapata matibabu kwa wakati anaweza kupungukiwa maji mwilini kutokana na kuharisha ambako kunaweza kusababisha kupoteza madini muhimu hivyo kuwa katika hatari ya kupoteza maisha, “ anasema Dk Katoto.
Madhara mengine yanayoweza kujitokeza endapo ugonjwa utachelewa kutibiwa ni kuhara damu kupindukia, kutapika, kusikia kizunguzungu, kukosa hamu ya kula na kupata homa kali.
 
Pia, mgonjwa atakuwa katika hatari ya kupata matatizo ya kujikunja kwa utumbo endapo bakteria wanaoeneza ugonjwa huu watakuwa wengi.
Mgonjwa pia anaweza kupata vidonda kutokana na kutoboka kwa utumbo baada ya kushambuliwa na bakteria hawa ambao wanaweza kusafiri hadi kwenye ini na kumsababishia uvimbe.
 
Kujikinga
Ugonjwa huu, kwa mujibu wa wataalamu hutibika na kupona kabisa. Inakadiriwa kwamba wiki mbili za matibabu kama mgonjwa husika amewahi matibabu zinatosha kumaliza tatizo hili.
Dk Katoto anasema mgonjwa anashauriwa kumaliza dozi atakayopewa ili kupona kabisa ndani ya muda aliopewa na daktari aliyemtibu.
 
Kuna baadhi ya watu wana tabia ya kukatisha dozi pindi wanapohisi kupata nafuu. Unapofanya hivyo unakuwa katika hatari ya kuumwa tena kwani ulipokuwa ukitumia dawa bakteria walidhoofika na unapoacha wanajijenga upya,” anasema Dk Katoto
Watu wanatakiwa kuchemsha maji ya kunywa ili kuweza kuua vijidudu vinavyosababisha ugonjwa, kuchimba vyoo, kunawa mikono baada ya kutoka chooni na kufunika chakula.
 
Unapoandaa chakula hakikisha unaosha matunda na mboga za majani kabla hazijaliwa. Fanya hivyo kwa maji masafi, yanashauriwa yawe yanatiririka kama vile ya bomba au sinki la jikoni.
Unashauriwa kuepuka kula matunda na mboga isipokuwa uwe umeziandaa mwenyewe au una uhakika na aliyeziandaa. Usinunue matunda yaliyomenywa na kuyala popote yanapouzwa.
 
Unapokuwa sehemu ya mbali na nyumbani hakikisha unakunywa maji au juisi za chupa pekee. Usipende kutumia vinywaji hivyo kutoka vibandani au migahawa ambayo hauna uhakika na usafi wake.
Ukikosa maji ya chupa, hakikisha unachemsha maji ya kunywa au unayatibu kwa dawa zinazoshauriwa kama vile waterguard au iodine. Haya ndio maji unayoshauriwa kuyatumia kuandaa juisi pia.
 
Unapokuwa sehemu ya mbali na nyumbani hakikisha unakunywa maji au juisi za chupa pekee. Usipende kutumia vinywaji hivyo kutoka vibandani au migahawa ambayo hauna uhakika na usafi wake.
Ukikosa maji ya chupa, hakikisha unachemsha maji ya kunywa au unayatibu kwa dawa zinazoshauriwa kama vile waterguard au iodine. Haya ndio maji unayoshauriwa kuyatumia kuandaa juisi pia.
 
Usinywe maziwa yasiyosindikwa na bidhaa zozote zitokanayo kwani vyombo vinavyotumika kuandaa wanaweza wasizingatie kanuni zote za usafi. Ikibidi yachemshe kabla hujayanywa ili kuwa na uhakika zaidi.
Epuka kula barafu na chakula kinachouzwa mitaani bila kuwa na uhakika wa maandalizi yake. Kikubwa Zaidi, nawa mikono kwa sabuni kabla ya kula na kila baada ya kujisaidia.
 
Haufahamiki
Victoria Adolph, mkazi wa Mbagala Mtoni Kijichi anasema alikuwa haufahamu ugonjwa wa amoeba hadi mtoto wake alipougua na kulazwa hospitalini.
“Mwanzoni nilikuwa nampa dawa za kufunga kuharisha nikijua ni mchafuko wa tumbo lakini haikusaidia na alilazwa baada ya kupoteza maji mengi na kutundikiwa dripu tatu. Hapo ndipo niliujua,” anasema Victoria.
 
Back
Top Bottom