1.Hakikisha unaosha miguu yako kila siku kwa maji safi na sabuni.
Katika kutimiza majukumu yako ya kila siku tunatembea sana toka sehemu moja kwenda nyingine, miguu inakuwa imepitia kwenye vumbi na uchafu kibao pale siku inapoisha. Fanya zoezi la kuiosha miguu yako ni sehemu ya utaratibu wako wa kila siku kabla hujalala hata kama hutaoga usiku huo (mmmmhh na joto hili.....!). Isafishe vizuri kwa sabuni huku ukizingatia zaidi sehemu za katikati ya vidole vyako. Futa miguu yako kwa taulo au kitambaa kisafi na kikavu kwa umakini zaidi ili unyevu wote uishe, usilale na miguu iliyo na unyevu ni mwanzo wa kuzalisha vijidudu vya kuleta harufu mbaya.