Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unatibu vipi ukavu wa nyayo?kuna watu ambao tayari wana asili ya ngozi kavu hivyo ni lazima wafanye kazi ya ziada kulainisha miguu.
1.Ukimaliza kuoga tu unahakikisha unapaka nyayo zako mafuta au lotion zenye moinsture.Usipake lotion zenye kemikali au alcohol huzidisha ukavu wa miguu.Paka hata mafuta ya watoto ambayo hayana kabisa kemikali.
 
2.Pia unaweza kuloweka miguu yako kwenye maji yenye juice ya limao,juice ya limao husaidia kuondoa zile dead skin
3.Paka miguu yako mchanganyiko wa kijiko kimoja cha olive oil na matone kadhaa ya limao.Changanya vyema kisha paka kwenye nyayo ili kuipa moinstrure yaani unyevu unyevu.
 
4.Unaweza kutengeneza scrub yenye mchanganyiko wa unga wa mchele,olive oil,veniger na asali.Unazifanyia scrub nyayo zako na huo mchanganyiko.
5.Ukishasafisha na kufuta miguu yako paka vegetable oil…mafuta kama hayo ya olive na mafuta natural kabisa ya nazi.
 
Kabla ya kulala Chukua mafuta ya vaseline ujazo wa kijiko kidogo cha chai na kamulia limao zima kisha koroga vyema huo mchanganyiko kisha paka kwenye nyayo zako.Fanya hivi ukiwa umenawa miguu na umeifuta vizuri imekauka ndio unapaka.Vaa socks zako ndio upande kitandani kulala.
 
Kabla ya kulala Chukua mafuta ya vaseline ujazo wa kijiko kidogo cha chai na kamulia limao zima kisha koroga vyema huo mchanganyiko kisha paka kwenye nyayo zako.Fanya hivi ukiwa umenawa miguu na umeifuta vizuri imekauka ndio unapaka.Vaa socks zako ndio upande kitandani kulala.
 
Magaga ya miguuni ni tatizo linalowakumba watu wengi na kuwafanya wasiwe huru kuvaa aina za viatu. Miguu inahitaji matuzo ikiwemo hewa ya kutosha.


Kama unataka kuzuia miguu yako isipasuke hakikisha unaisafisha mara kwa mara, tumia scrubs kusugua miguu yako kuanzia juu hadi chini safisha na maji ya uvuguvugu au unaweza kutumia shampoo tu kisha paka mafuta ya olive oil au mafuta ya nazi.
 
Ukiwa na magaga au nyayo ngumu hakikisha unaiosha mara kwa mara na kuisugua kwa kutumia kifaa maalum, nenda duka la vipodozi uulizie kifaa cha kusafishia nyayo kisha nunua mafuta au losheni maalum ya kulainishia miguu yako.
 
Njia rahisi ya kuosha miguu ukiwa nyumbani, loweka miguu yako kwenye maji ya uvuguvugu yenye chumvi au unaweza kuweka shapoo baada hapo sugua kwa kifaa maalum cha kusugulia miguu ukisha maliza kausha miguu yako kwa kitaulo maalumu baada ya hapo pakaa mafuta ya maji au losheni kwa kutumia njia hii utafanikiwa kuondoa mipasuko katika miguu yako .
 
Magaga ni ugonjwa unaosababisha miguu kupasuka na wakati mwingine kufikia hatua ya kutoa damu. Leo ninawaletea tiba inayoweza kutibu tatizo hilo kwa kutumia chakula.
UNGA WA MCHELE
Wengi wameuzoea unga wa mchele kwa kupikia vitumbua, wengine hutumia kwa kuchanganya na unga wa mahindi ili kupika ugali na baadhi hupikia mikate.
Hayo ni matumizi ya kula, lakini kwa upande wa tiba husaidia kuondoa mpasuko wote wa gaga.
 
MAHITAJI
Kijiko kimoja cha asali, unga kiasi wa mchele, siki ya tufaha kijiko kimoja kidogo.
Ukimaliza changanya vyote kwa pamoja ili kupata mchanganyiko mmoja, kama miguu yako itakuwa imepasuka sana mpaka imefikia kutoa vidonda, changanya mchanganyiko huo na mafuta ya mrozi au ya mzaituni.
Baada ya hapo paka mchanganyiko wako kwenye mpasuko, kisha acha kwa muda wa dakika kumi, kisha chukua unga wa mchele uliolowekwa kwenye maji kidogo, uwe mzito kisha upake tena kwenye nyayo zako. Ukikauka sugua kama unafanya masaji, fanya hivi kila siku mpaka utakapoona tatizo limeisha.
 
Mafuta ya nazi ni mazuri kama yatatumika ipasavyo.yana uwezo wa kukufanya uonekane mrembo mwenye ngozi ya kuvutia.

MAKE UP REMOVAL/KUONDOA MAKE UP

mafuta ya nazi yanaweza pia kutumika kuondoa makeup usoni baada ya kutoka kwenye sherehe ukiwa na makeup unashauriwa kuitoa kabla ya kuingia kulala ili kuendelea na ngozi nzuri yenye afya.
mafuta ya nazi yanatumika hivi
chukua pamba safi chovya kwenye mafuta ya nazi.
 
kisha anza kufuta uso wako taratibu kwa kutumia pamba iliyo na mafuta ya nazi.
baada ya kufuta chukua cleanser uliyoandaa au nawa uso wako vizuri na sabuni.
ukifanya haya utasaidia kutunza uso wako na kuwa na afya nzuri.

KULAINISHA NGOZI

Mafuta ya nazi pia hutumika kama kilainishi kwa ngozi yako especially :
kuondoa magaga kwenye nyayo za miguu
kuzuia mipasuko ya nyayo za miguu
kukauka kwa ngozi ya mikononi
hivyo mafuta yanazi yanasaidia kwa kiasi kikubwa sana kulainisha ngozi na kuipa afya nzuri.
 
Back
Top Bottom