Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1. Anawinda kwa akili sana pengine kuliko anayewindwa. 2. Anaweza kukukamata hata akiwa usingizini kwani huwa na tabia ya kutofunga jicho moja anapolala na jicho hilo hutambua kila kinachoendelea. 3. Anapokuwa majini akiwa anakunyatia unaweza usitambue kwani huyaacha maji tulivu. 4. Nchi kavu unaweza kumuonea onea ila kwa wakati wote atakuwa anafanya timing akutangulize majini.
 
5. Anaweza kukumaki, kwa mfano ukiwa na tabia ya kuoga au kuchota maji saa kumi sehemu flani katika mto au ziwa kuna siku atajificha hapo hata nusu saa kabla. 6. Akifanikiwa kukujeruhi tambua umekwisha kama msaada wa watu utakuwa mbali, hata akikuacha dakika kumi. 7. Anapambana kwa mdomo na mkia. Kama ilivyo kwa Mamba Fisi naye ana mbinu zake za uwindaji :-
 
1. Anawinda kwa pupa huku akikuathiri kisaikolojia kwa kukutisha na kelele za ajabu. 2. Anapokuwa na njaa Kali huwa anaongeza nguvu ya mapambano na wakati huu huwa haofii muonekano wa anachotaka kuwinda. 3. Akikosa windo na mizoga, chakula hupata kwa njia za uporaji. 4. Ni bingwa wa mbio za taratibu katika masafa marefu, ukimkimbia atakukamata mbele ya safari ukiwa hoi umechoka. 5. Anaposhindwa zoezi lolote huwaita wenzie kwa ishara, wakati huo wewe utakuwa unamshangaa fisi anacheka.
 
Kama wewe ni miongoni mwa wanaowachukia wanyama hawa basi kaa ukijua unaungana na Mfalme wa poli bwana pantela Leo (simba), kwani viumbe hawa humkosesha raha kuliko kung'atwa na fisi yupo radhi amuachie nyama aliyowinda kwa tabu, na hata anapopambana hao mara nyingi hukunja miguu yake ya nyuma kwa maana ya kumuachia aume popote lakini sio mdomo wake ufikie mguuni, simba wa watu anaogopa ulemavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…