Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

WAJUE NDEGE
NDEGE ni aina ya mnyama. Tofauti ya ndege na wanyama wengine ni kwamba ndege ana mabawa yanayomwezesha kuruka angani aidha ndege hutaga mayai
Ndege wako wa aina nyingi, wakubwa na wadogo ni kama Tai, Mbuni, Korongo, Bata mzinga, Bundi, Tausi, Mwewe na wengine wengi.
Ndege wadogo wengine ni kama tetere, Mbayuwayu, Jorohe, Kasuku, Charwe, Chiriku, Kwelea kwelea, na wengine.
 
MAISHA YA NDEGE
Maisha ya ndege hutegemea sana mazingira. Mazingira mazuri huwafanya ndege kuishi kwa amani, furaha mustarehe. Mazingira yakiharibiwa husababisha ndege huhamia mahali pengine au kuwa waharibifu.
Ndege hupendelea kuishi mahali pa utulivu na panapovutia. Idadi na aiana toafauti za ndege ni moja ya ishara zinazoonyesha kuwepo kwa mazingira bora. Umri wa kuishi ndege hutfautiana kama zilivyo aina zao, lakini kuna baadhi ambao hufikia kuishi miaka 15.
 
MAKAZI YA NDEGE
Ingawa ndege huishi kwenye mazingira tofauti kulingana na aina au jamii husika. Lakini wengi huishi misituni.
Ndege wengi hujenga viota hasa misimu ya kuzaliana. Viota hivi hujengwa kwa kutumia majani, dongo na vijiti. Vilevile wapo ndege waishio mapangoni.
Viota vya ndege hujengwa kwa ustadi mkubwa ili kuwakinga na baradi, mvua, maadui na upepo mkal wakati wa kuzaliana. Ndege wengi hutumia viota kwa kuzaliana si kuishi.
 
Ndege hupendelea kujenga viota vyao juu ya miti, ndani ya mapango, kwenye paa au kona za nyumba ili mradi tu sehemu hizo ziwe za usalama. Aidha mahali hapo ni lazima pawe pana maji, chakula, upepo, na pia mandhari mazuri.
Ndege wengine hupendelea kuishi majini, kwa mfano batamaji. Wengine hupenda kuishi kwenye ardhi owevu.
 
UZAZI WA NDEGE
Kwa kawaida ndege jike hutaga mayai ambayo huangaliwa na kup[atikana kwa kinda. Kabla ya hapo ndege dume na jike hujamiiana ili kurutubisha mayai. Ndege hawanyonyeshi hivyo makinda hukua kwa kuletewa vyakula na wazazi wao wanaovipata kwenye mazingira yanayowazunguka. Idadi ya mayai hutofautiana na aina ya ndege. Kuna wanaotaga mayai mawili kama njiwa na wengini mayai mengi kama mbuni.
 
Baada ya kutaga jike mara nyingi hulazimika kuatamia mayai kwa siku kadhaa kabla ya makinda kuanguliwa. Siku za kuatamia hutofautiana kulingana na aina ya ndege. Wapo wanaoatamia kwa siku 14, 21, 42 au zaidi. Walio wengi huatamia kwa siku 21.
Wakati wa kuatamia mayai ndege jike hulazimika kukaa kiotani bila ya kula chakula kwa muda Fulani kwa nia ya kuyapa joto mayai. Hali hii hufanya jike kunyonyoka manyoya na hata kukonda. Jike hunyonyoka manyoya sehemu za tumboni ili kuweza kuyapasha joto mayai yake vizuri.
 
Wakati mwingine ndege dume hulazmika kuleta chakula kiotani ili kumlisha jike. Baadhi ya ndege dume husaidia kuatamia mayai jike anapokwenda kujitafuatia chakula. Makinda wanapoanguliwa huwa hawana uwezo wa kuruka kwani mabawa yao hayana manyoya, hivyo hubaki kiotani. Kwa wakati huo jike na dume husaidiana kulinda makinda wao mpaka watakapomudu kuruka na kujitafutia chakula.
 
CHAKULA CHA NDEGE.
Ndege hula vyakula vya aina mbalimbali kama vile nafaka, wadudu, mizigo, matunda, majani, samaki, mabaki ya vyakula nekta nakadhalika.
Ulaji wa vyakula hivi hutegemeana na aina ya ndege na maumbile yake. Kwa mfano ndege wenye midomo iliyochongoka hunyonya nekta ya maua. Ndege aina ya Tai hula mizoga; hawa midomo yao ni mikubwa na imara Aidha ndege pia hutumia kucha zaokujipatia chakula kwa njia ya kuchakua. Wengine hutumia mdomo yao na kucha zao kwutafuta wadudu , samaki, na hata wanyama wadogo wadogo.
 
Back
Top Bottom