Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Maumbile ya Ndege.
Ndege hutofautiana kimaumbile. Ipo tofauti kati ya Dume na Jike pia makinda. Kwa mfano Tausi dume ana rangi nzuri zaidi kuliko jike na mkia wake ni mrefu na wenye urembo mwingi na rangi nzuri.
Njiwa jike huwa na mdomo mrefu kuliko njiwa dume. Bundi jike shingo yake ni nyembamba wakati ile ya dume ni nene.
 
Wakati mwingine ukubwa wa vichwa hutofautisha ndege jike na dume. Jike huwa na kichwa kidogo ambapo dume chake ni kikubwa. Baadhi ya ndege dume huwa na ushungi juu ya vichwa vyao.
Mara nyingi dume huwa na umbile kubwa na rangi za kupendeza kuliko jike.
Ndege wana manyoya mazuri yenye rangi za kuvutia kwa mfano, Tausi, Kanga, Kasuku, na wengine kwa sababu hii manyoya yao hutumika kwa mapambo. Ndege wana sauti tofauti kama walivyo wanadamu. Sauti za ndege huburudisha, kama vile ile ya Chiriku.
 
Nyimbo za ndege huwa na maana na ujumbe fulani.Madhalani ndege dume aimbapo huashiria jike kwamba ‘liko dume bora hapo’. Madume wengine wasingilie himaya yake vinginevyo vita vitazuka.
Baadhi ya sauti huashiria hatari na kutoa tahadhadhari. Baadhi ya ndege huimba kwa muda mfupi huku wakibadilisha sauti, wakati wengine hawawezi kubadilisha sauti. Chiriku anaaminika kuwa ndege mwenye sauti nzuri zaidi ya wengine.
 
Sauti za ndege pia huoanishwa na matukio katika jamii mbalimbali. Kwa mfano Bundi kwa jamii nyingi za kiafrika huaminika kuwa ni ndege wa uchuro. Lakini Ulaya bundi ni ndege wa busara.
Ndege huhama kutoka sehemu mmoja kwenda nyingine. Sababu za uhamiaji huo ni kutafuta chakula, maji, mabadiliko ya hali ya hewa na kuharibiwa mazingira yao. Pia hutafuta sehemu za kuzaliana.
 
Back
Top Bottom