Wakati mwingine ukubwa wa vichwa hutofautisha ndege jike na dume. Jike huwa na kichwa kidogo ambapo dume chake ni kikubwa. Baadhi ya ndege dume huwa na ushungi juu ya vichwa vyao.
Mara nyingi dume huwa na umbile kubwa na rangi za kupendeza kuliko jike.
Ndege wana manyoya mazuri yenye rangi za kuvutia kwa mfano, Tausi, Kanga, Kasuku, na wengine kwa sababu hii manyoya yao hutumika kwa mapambo. Ndege wana sauti tofauti kama walivyo wanadamu. Sauti za ndege huburudisha, kama vile ile ya Chiriku.