Mnyama huyu ana miraba mingi myeusi ya mkato usoni na miguuni.Pundamilia ana nywele ndefu kati ya masikio na ukwato mmoja kama wa Farasi na kihongwe ambao ni jamii yake.
Mistari ya Pundamilia humsaidia kujificha kutokana na maadui zake.Inaweze kuwa rahisi sana kumuona Pundamilia katika maeneo ya kawaida ya binadamu,lakini awapo porini hasa kukiwa na mwanga mwingi au giza si rahisi kwa adui kumuona kwa urahisi.
Mistari hiyo ambayo hutofautiona kutoka Pundamilia mmoja hadi mwingine huhuisha ulinzi dhidi ya maadui zake ambao adui huyo hawezi kumchukua Pundamilia mmoja katika kundi lake kwa urahisi.Kwa sababu huonekana kama wanafanana sana.
inasemekana chimbuko la pundamilia hasa ni kusini mwa Afrika na wao hupendelea zaidi kuishi kwenye maeneo ya mbuga na nyika.Pundamilia ni mnyama anaependa umoja na ushirikiano nawanyama wengine.Mara nyingi utamkuta na Swala,Twiga,Nyumbu n.k.
The reason why the wedding ring is placed on the fourth finger of your left hand is because it's the only finger that has a vein linking directly to your heart.