Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tabia ya kushangaza ya mnyama huyu,hupendelea kuishi katika familia yenye Pundamilia (5) watano hadi Ishirini(20) ambapo ,Pundamilia dume moja na majike kadhaa pamoja na Pundamilia wadogo huishi pamoja.Dume ndilo huwa na dhamana ya kuilinda familia hiyo na maadui.
 
Pundamilia ni mnyama mpole,mtulivu,mwenye huruma na ushirikiano.Mmoja wao akiugua na kushindwa kutembea kwa haraka ,kundi la familia hiyo hupunguza mwendo ili kuenenda pamoja na mwenzao ambaye ni mgonjwa.Aidha mmojawapo anapopotea familia hiyo huchukua jukumu la kumtafuta kwa siku kadhaa.
 
Screenshot_2017-09-13-23-56-57.png
 
Hata hivyo,familia zenye pundamilia watano hadi 20 huungana na familia nyingine na kufanya kundi kubwa na kila kundi huwa na mpangilio wake.Pundamilia wazee hushabihiana kwa kiasi kikubwa lakini madume na majike mara nyingi hutengana na familia zao na kuunda familia nyingine.Aidha baadhi ya Pundamilia dume ambao hawana familia huungana na kuunda kundi la 'makapera'.
 
Pundamilia huwa makini sana wakati wa mchana,wakati wa usiku hupendelea kula sehemu zenye nyasi fupi ili kujikinga na maadui.Hutumia muda kama saa moja hivi kula na kutembeatembea.Wakiwa katika mapumziko baadhi ya Pundamilia hulala na mmoja hubakia kasimama akiwalinda wenzake na maadui ambao wanaweza kujitokeza.
 
Back
Top Bottom