Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

tapatalk_1505229578444.jpeg
 
PASINA shaka kwamba uwezo wa kuwasiliana ni mojawapo ya zawadi zenye thamani zaidi ambazo wanadamu walipewa. Kwa kutumia uwezo huo, sisi huwasilisha habari muhimu kwa wanadamu wenzetu iwe ni kwa maneno ama bila kusema, kama vile kwa kutumia ishara. Kotekote ulimwenguni, watu hupigania uhuru wa kusema. Hivyo, watu fulani wamefikiri kwamba wanadamu peke yao ndio wanaoweza kuwasiliana.
 
Hata hivyo, uchunguzi unaonyesha kwamba wanyama huwasiliana kwa njia tata ambazo mara nyingi ni vigumu wanadamu kuzielewa. Naam, wanyama “huzungumza,” si kwa maneno, bali kwa ishara. Ishara hizo zatia ndani kutikisa mkia, sikio, au kupigapiga mabawa. Njia nyingine za mawasiliano zahusisha kutumia sauti, kama vile kubweka, kunguruma, au sauti za ndege wanapoimba. Wanadamu wanaweza kutambua “lugha” fulani za wanyama kwa urahisi, lakini nyingine zaweza kutambuliwa tu baada ya uchunguzi mwingi wa wanasayansi.
 
Wanyama Wanaowinda!

Ni katikati ya mwezi wa Julai. Katika Mbuga ya Taifa ya Serengeti huko Tanzania, maelfu ya nyumbu wanaelekea kaskazini kwenye Mbuga ya Wanyama ya Masai Mara nchini Kenya ili kutafuta malisho. Milio ya kwato zao inasikika kwenye nyanda, huku wakiendelea na uhamaji wao wa kila mwaka. Hata hivyo, kuna hatari mbalimbali njiani. Kuna wanyama wanaowinda, kama vile simba, duma, fisi, na chui. Nyumbu hao bado watahatarisha uhai wao kwa kuvuka Mto Mara ulio na mamba wengi. Nyumbu hao huwaepukaje wanyama wanaowinda?
 
Ili kumkengeusha adui, nyumbu hukimbia umbali mfupi kwa kasi kisha yeye hugeuka ili kumkabili adui, huku akitikisa kichwa chake huku na huku. Nyumbu huyo hurukaruka kwa njia ya ajabu na ya kuchekesha. Hata mnyama mkali sana huzubaa anapoona mchezo huo wa kiajabu. Mnyama anayewinda akiendelea kumkabili, nyumbu huyo huendelea kurukaruka. Jambo hilo humvuruga mnyama anayewinda na laweza kumfanya amwache nyumbu na kuondoka. Mchezo huo wa kiajabu wa nyumbu umemfanya aitwe mcheshi wa nyanda.
 
Back
Top Bottom