Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Inzi ana mabawa mawili na miguu sita ambayo pia huitumia kuonjea chakula. Miguu ya nzi ina uwezo wa kuonja sukari mara milioni 10 haraka zaidi ya ulimi wa mwanadamu!!. Inzi hutumia milingoti (antenae) yake kunusia. Ingawa inzi ana lensi 4000 ndani ya macho yake, lakini huona vizuri umbali wa inchi 24 hadi 36.
 
Sehemu nzuri za inzi kutagia mayai ni zenye unyevunyevu mchafu, wenye joto na vitu vilivyooza kama vyooni hasa vya shimo, jalalani, n.k. Mama inzi mmoja mwenye afya nzuri anaweza kutaga mayai 50 mpaka 75 kwa mtago mmoja hadi mayai 500 – 1000 kwa maisha yake yote.
 
Kukupa tu wazo jinsi inzi wanavyoongezeka kwa haraka, kulingana na hekima za mtaalamu wa wadudu (entomologist) mmoja aitwaye Hodges: wakiwepo inzi wawili (baba na mama) wenye afya nzuri, wakianza kazi Aprili; ifikapo Augosti, inzi hawa watakuwa wametengeneza jeshi la inzi wengine wapatao 191, 010, 000, 000, 000, 000, 000!!!.
 
Vijichanga vya inzi au viwavi (larvae or maggots) ni vyeupe ambayo hubadilika kiukuaji (pupate) na kuwa inzi kamili, ambaye huweza kuishi (lifespan: hatch to dispatch) kwa wiki mbili hadi mwezi mmoja kulingana na mazingira. Inzi hupitia metamorphosis (mtafsiri tafadhali) na maisha kamili ya aina nne (lifecycles – progress from egg to actual housefly) yaani kama yai (egg), larva or maggot, pupa na kisha inzi kamili. Yai hukaa hadi siku moja na kuanguliwa kuwa kiwavi; kiwavi hukaa hadi wiki moja na kubadilika kuwa inzi kamili.
 
Wataalamu wanadai kuwa kuna zaidi ya aina 87, 000 za inzi (sio wa nyumbani tu) duniani; lakini inzi wa nyumbani (housefly) ninayewazungumzia hapa ndiwe wengi, karibu asilimia 91 ya nzi wote wanaoishi mazingira ya wanadamu (domestic).
 
Inzi si mdudu mzuri kama tunavyojua na tulivyoona awali kwa sababu ni mleta magonjwa mengi yanayotesa duniani kote. Baadhi ya magonjwa yanayosabishwa na inzi (samahani mengine siyafahamu kwa Kiswahili – anayeweza atanisaidia) ni pamoja na homa ya typhoid, homa ya manjano (yellow fever), kifua kikuu (tuberculosis), ukoma (leprosy), kipindupindu (cholera), kuharisha (diarrhoea), minyoo (parasitic worms), dysentry, anthrax, bubonic plague, scalet fever, yn.k.
 
Inzi wanaweza kubeba chembe chembe zinazoweza kusababisha magonjwa (disease causing microorganisms) ndani na nje ya miili yao. Inzi mmoja anaweza kubeba hadi chembe chembe milioni mbili na hivyo kuwa sababu ya magonjwa ya mlipuko. Ukimwona ametua kwenye mkono wako au kwenye kikombe chako cha chai, anaweza kuwa kaacha mamilioni ya chembe zinazoweza kukupa maradhi ya kutisha; inzi ni hatari kwa afya yako na familia yako.
 
Ingawa inzi ni kati ya wadudu wanaoruka upesi sana (4½ mph), mara nyingi hawasafiri mbali na walikozaliwa, ingawa upepo unaweza kuwabeba mbali. Inzi hupenda sana harufu mbaya na mazingira machafu; hivyo ukitaka wakutembelee, harufu mbaya ni kadi mojawapo nzuri ya kuwaalika.
 
Back
Top Bottom