MFAHAMU FISI. Fisi ni myama aishiye mbugani, ambaye ana sifa kemu kemu kwa wanadamu, pengine hii ni kutokana na kutokeza katika simulizi nyingi tulizokuwa tukijifunza katika hadithi, pindi tulipokuwa shule ya msingi, ana umaarufu wa jina la bwana afya wa porini, hii ni kutokana na sifa yake ya kula mizoga, lakini pia ni mnyama ambaye amepata sifa nyingi za kuwa bwege kutokana na kusumbuliwa sana sungura katika hadithi hizo za shule ya msingi.