Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

NIKUPE VIONJO KADHAA KUHUSU MASHOTO
1. Mashoto wana uwezo mkubwa sana wa kutunza kumbukumbu kiasi kwamba wengi wao hawatumii shajara (diary) na hawapendi kutumia notebooks wanapomsikiliza mtu akitoa mhadhara. Utagundua kuwa katika maisha yako ya shule wengi wa MASHOTO ambao ni vipanga si wasomaji wa kukomaa sana/kukesha nk.
 
2. Mashoto wengi duniani wana miandiko (handwriting) mizuri na yenye kuvutia mno. Na wanao uwezo mkubwa wa kuandika maandishi (herufi na tarakimu) kwa kinyume (toka kulia kwenda kushoto)

3. Mashoto wana vipaji vingi zaidi. Mashoto mmoja anaweza kuwa mchoraji, mshairi, mcheza mpira, mchonga vinyago, mwandishi wa hadithi, mbunifu wa mitindo, mbunifu wa bustani, mcheza filamu, mpigapicha, mpambaji, mwanamuziki na vingine vingi. Tizama mfano wa wanasoka wengi mahiri duniani waliopita waliopo na wajao ni MASHOTO na hii pia inagusa kwa michezo mingine kama Tenis na Ndondi (boxing)
 
4. Kwa mujibu wa utafiti wa Dr. Alan Searleman wa Chuo Kikuu cha Mt. Lawrence huko New York, Marekani, mashoto wana uwezo mkubwa zaidi wa utatuzi (problem-solving skills). na kwamba asilimia kubwa ya watu wenye IQ kubwa ni MASHOTO. Katika wabunifu watano wa kwanza wa kompyuta za Mcintosh, wanne kati yao walikuwa mashoto.
 
5. Viongozi wengi mashuhuri duniani waliopita waliopo na wajao ni MASHOTO. Katika marais wanne wa hivi karibuni wa Marekani, marais watatu ni mashoto. Tazama, George Bush mkubwa (mashoto), Bill Clinton (mashoto), George Bush mdogo (kulia) na Barack Obama (mashoto). Na, katika uchaguzi wa urais wa Marekani wa 1992, wagombea wote watatu wakubwa walikuwa mashoto. Uchaguzi wa Marekani wa 2008, wagombea wote wawili Obama na McCain walikua ni mashoto.
 
1505580299283.jpg
 
6. kwa ujumla. Mashoto wanaelezwa kuwa na uwezo mkubwa sana wa utambuzi (perception). Watafiti wanaeleza pia kuwa mashoto wana mhemuko, mchomo wa moyo ama hisia (emotions) kwa kiasi kikubwa zaidi. Hivyo mashoto wanaelezwa ni watu wenye upendo na huruma kwa kiwango cha hali ya juu sana.
 
Back
Top Bottom