Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
katika mikoa mengine kama vile pwani, Lindi, Morogoro,Tanga na Mtwara tofauti na watu walivyofikiria zamani kwamba kunguru wanasafisha miji ukweli ni kwamba wanachafu zaidi kwa kutapanya au kutawanya mabaki ovyo sehemu mbalimbali. Hata hivyo kunguru hulala popote ila wanapokaribia kutaga mayai na hupenda kujenga viota vyao juu ya mti au jabali na hutumia vijiti na majani,kunguru ni miongoni mwa ndege wenye mfumo sawa wa kijinsia kwa kuwa dume na jike hushirikiana kujenga kiota maalumu kwa ajili ya mayai na makinda na kiota cha ndege hawa aina ya kunguru hujenga kiota kwa siku nane hadi kumi na nne kati ya mwezi Julai na Machi.