Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

katika mikoa mengine kama vile pwani, Lindi, Morogoro,Tanga na Mtwara tofauti na watu walivyofikiria zamani kwamba kunguru wanasafisha miji ukweli ni kwamba wanachafu zaidi kwa kutapanya au kutawanya mabaki ovyo sehemu mbalimbali. Hata hivyo kunguru hulala popote ila wanapokaribia kutaga mayai na hupenda kujenga viota vyao juu ya mti au jabali na hutumia vijiti na majani,kunguru ni miongoni mwa ndege wenye mfumo sawa wa kijinsia kwa kuwa dume na jike hushirikiana kujenga kiota maalumu kwa ajili ya mayai na makinda na kiota cha ndege hawa aina ya kunguru hujenga kiota kwa siku nane hadi kumi na nne kati ya mwezi Julai na Machi.
 
Baadhi ya kunguru hutumia kiota kwa mfumo wa ujamaa ambapo kiota kimoja, kunguru jike hutaga mayai kati ya matatu hadi kumi, mayai hayo yanarangi ya kijani kilichopauka na madoa ya kahawia wakati wa kutumia dume hufanya kazi ya kumtafutia chakula kunguru jike jambo ambalo linasababisha watalaamu kuwaweka ndege hao kati kundi linalogawana kazi kwa kuziangalia usawa. Japo kuwa kunguru hutamia kwa muda wa siku 18 na makinda ya kunguru hutoka nje ya kiota baada ya wiki 10 kulingana na aina ya wengi hutoka nje baada ya wiki moja ila wanaendelea na kukaa chini ya uangalizi hadi wanapofikisha umri wa mwezi mmoja,kunguru ana uwezo wa kuishi kwa wastani wa miaka mitano hadi kumi. Hata hivyo baadhi ya utafiti uliofanywa na watafiti wakubwa duniani kote zilisema kuwa kunguru mwitu wana uwezo wa kuishi maisha mafupi zaidi kwa kuwa wanazunguukwa na adui wengi kunguru hutoa milio mbalimbali na baadhi ya
 
watafiti wa maisha ya ndege walidai kuwa kunguru wana uwezo wa kufanya mawasiliano kutumia lugha maalumu. Watafiti hao wanapingana kuhuaiana na lugha maalumu ya kunguru wanauwezo wa kujifunza kuitika milio ya wanyama wengine na tabia hii hubadilika kwa misimu kadhaa,milio ya kunguru ni migumu kuelewa. BAAD YA KUFAHAMU MAMBO MBALIMBALI,TUANGALIE MADHARA YA NDEGE KUNGURU. Japokuwa kuna faida,na umuhimu wa ndege kunguru,hizi zinazofuata ni madhara ya ndege kunguru, ndege huyu ana matatizo makubwa sana katika jamii ya watu. Inasemekana kuwa kunguru huangusha mbegu ngumu kwenye barabara na kusababisha magari yanaporuhusiwa kukanyaga mbegu hizo na husababisha matairi kupasuka na kupata ajali,kunguru wanasifa ya kuharibu miundombinu kama vile nyaya za umeme na za antena za runinga. Kunguru husababisha kero na adha kubwa kwa wakazi katika sehemu mbalimbali wanakopatikana ikiwa ni pamoja na tabia yao ya kudokoa vyakula kubeba vitu ving'aavyo ikiwa ni pamoja na pete,hereni na simu za mkononi,vijiko,visu na vipande vya chuma na vitu vyenye harufu.
 
Ripoti ya utafiti wa hivi karibuni zinaonyesha kuwa kunguru wana uwezo mkubwa wa kutambua watu wanaokutana nao katika mazingira tofauti kila siku. Katika utafiti huo watu waliogawana katika makundi mbalimbali ambapo kundi moja lililenga urafiki na kunguru kwa kuwapa chakula na kundi lingine lilijenga uadui na kundi lingine baada ya ya siku kadhaa,kunguru hao waliweza kuangusha na kutambua wale waliowapiga na waliowapa chakula kufuata na waliowapiga waliwakimbia kila wanapowaona.
 
Kwanza uchumba halafu harusi/ndoa.

Katika mila za wangoni, hapo zamani kijana na msichana wakikua kufikia umri wa kuoa walioa. Kwa mila za wangoni, mtoto wa kiume hata kama akikua na kuoa halafu hajaenda vitani ilikuwa haionyeshi maana. Wakati wa kupigana vita kijana ilibidi aonyeshe nguvu zake zilivyo. Kijana ambaye bado hajaenda vitani aliitwa (walimwita) ”lijaha” ikiwa na maana ya kijana/mvulana mdogo. Kijana ambaye ametoka vitani walimwita/aliitwa ”lidoda” ikiwa na maana mkubwa . Mke wa kuoa walimtafuta ambaye ni mwenye ukamilifu, anayejua kufanya kazi za nyumbani. Anatafutwa mwanamke anayeweza kuokota kuni, kuchota maji, kutwanga, kupika chakula, kupika pombe na awe mwanamke anayecheka vizuri na watu wote katika mji.
 
Ndoa haifungwi katika ukoo. Kwa wangoni hawaoi mke au kuolewa na mume mwenye (kibongo) ubini mmoja. Kama watu wakioana katika ukoo, basi wazee wataulizia kwanza kama ukoo huo ni wa karibu au wa mbali. Kama hawa watu walioana katika ukoo wa karibu, basi watawaapizia. Watu wnaogopa kuoana ndani ya ukoo kwasababu wakifanya hivyo watoto watakaozaliwa watakufa. Na pengine watoto hao watapata kifafa au pengine mababu (mahoka) watakasirika.
 
Kulonda mdala=Kutafuta mke:-
Wenye mtoto wa kiume wanapotaka kumwoza kijana wao , wazazi wengine walimtafutia mke. Wazazi wengine walimwacha kijana wao atafute mwenyewe mke. amtakaye. Kama walimwona msichana mrembo watamtafuta ndugu yao ambaye watamtaka na kumwelezea habari za ndoa. Na huyu ndiye atakayekuwa MTENGA wao.
 
Mtenga huyu ataanza kuulizia kwa siri mambo ya wazazi wa msichana yule na wanaukoo wake wote na halafu ataenda kuwaeleza wazazi wa kijana. Kama wazazi wataona ya kuwa ni msichana wa hodari, watenga wale wataenda kwa wazazi wa msichana na kuuliza kama wanaruhusiwa kumwoa? Kama wenye binti watakataa, watenga wataombeleza.
 
Kujitokeza:- Ni lazima wawe na kiulizio , watenga ndio wataenda kuulizia kumwoa mke. Wanapoenda kule , wanachukua kitu fulani ”lukotelu au luhongelu” ni kiulizio , kitu hicho chaweza kuwa nguo, ushanga au hela nk.
 
Chiyagabuli= Mahari ya mwanzo

Kama wakwe wa pande zote mbili wanakubaliana watoto wao waoane, watenga watapeleka mahari kidogo kwa mama na baba wa binti ambayo ni mahari ya mwanzo. Baada ya muda yatapelekwa tena mahari ya mwanzo yaani kwa mara ya pili itakuwa jembe moja LUSUKA. Kama aina fulani ya jembe "ngwamba" ni jembe lenye tundu pale pmini unapotumbukizwa. Hii itamaanisha binti yao tayari amekwisha poteza ubikira
 
Kuchicha= kumtembela mchumba
Kuchicha ni kitendo cha msichana aliyechumbiwa kwenda rasmi kumtembelea mchumbake, kimila huyo msichana aliyechumbiwa anaenda na rafiki yake wa kike. Hivyo basi siku hiyo inakuwa ni kama anaenda kuona mazingira atakayokuja kuishi. Kimsingi katika siku ya kuchicha hairuhusiwi kulala pamoja na kufanya mapenzi ndio maana msichana alipaswa kusindikizwa na msichana mwenzake.
 
Lakini basi mara nyingi imekuwa ngumu kujizuia wengi wamekuwa wakiishia kufanya mapenzi, mbaya zaidi unakuta mvulana anaalika na mvulana mwenzake halafu wanagawana hao wasichana waliofika hapo. Lakini pia hilo neno limekuwa likitumika isivyo rasmi kama vile kitendo cha msichana kutongozwa na mvulana wapo walioita kitendo hicho kuchicha na imezoeleka na wengi.
 
Au pia inakuwa kinyume:- Kijana wa kiume pamoja na vijana wenzake wanaenda rasmi kumtembea mchumba/msichana. Huko anafanya kazi nyingine nyingi. Kwa kufanya hivyo, wakwe watamwona ni kijana /mume wa uhakika, kuwa anaweza kufanya kazi za kianaume, kama anajua/weza kulima kukata matema(kukata miti shambani kwa ajili ya kuandaa shamba), kama ana kaa/ishi vizuri na watu au kama hana haraka ya kula.
 
Muda wote huo wa aliokuwepo, kijana huyu hajionyeshi kwa wakwe zake. Anapotaka kutoka nje ya nyumba alalayo ni lazima ajifunike nguo usoni gubigubi. Kijana atafanya hivyo atakapotaka kumwona mtarajiwa mkewe, hakuna kujionyesha kwa wakwewe mpaka atakapozaa mtoto. Na mwanamke atafanya hivyo kwa wazazi wa mumewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…