Mbwa Mwitu.
Ukiwaona huwezi kuwazania ni wanyama wadogo sana wanaokula nyama na wawindaji, katika umbo hata fisi ni mkubwa kwao, wana heshima kubwa hawa jamaa si fisi wala simba huwa wanawaheshimu, wakiwa na nyama wanawaachia bila shuruti, ubabe wao huwa kwakuwa wanatembea kwa makundi makubwa kama vibaka wa panya road, maisha yao ni mpera mpela usikosee ukapita jilani yao una damu umekwisha, hawapatani na damu kabisa wakiiona tuu majini yao huamka, hata mwenzao wanaweza kumla, vidogo vina nguvu, wakati mwingine huangusha hata wanyama wakubwa, tabia yao ni kung’ata akitoka na nyama anakula kisha anafuta mdomo anarudi tena kuifata, sifa yao nyingine ni mbio wanauwezo wa kukimbia umbali wa km 71 kwa saa moja tuu.