Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

VYAKULA WANAVYOPENDELEA **********************
Mbwa mwitu ni wanyama wanaokula nyama na wanyama wanaopendelea kuwawinda ni pamoja na paa, mbawala, nyumbu,pundamilia nk pamoja na wanyama hao lakini pia huweza kuwawinda wanyama wakubwa ambao hata simba huwaogopa kama nyati na twiga nk. Mbali na nyama vijamaa hivi pia hula matunda ya polini pamoja na majani ambayo hutumia kama dawa pindi wajisikiapo wagonjwa.
 
SIFA ZAO ZA KIPEKEE***********
1. Maisha yao ni mpela mpela, hakunaga muda wa kupumzika muda wa kazi kila kitu ni mchaka mchaka tuu, wanaharaka pasina mfano.
2. Wanaamini katika ujamaa
3. Ni marufuku kujipaka damu wakati wa kula, na atayepatikana na damu wenzie humtafuna pia.
4. Wanapokula hunyofoa nyama hula, hujifuta damu kisha hufata nyama tena.
5. Wanaokula hutenga chakula cha watoto, sasa wewe na ukubwa wako jalibu kula utaiaoma.
 
6. Ukimpiga mmoja akakimbia dakika tano nyingi atarudi na kundi na utajuta kuzaliwa, nyati huwa wanaelewa sana kinachowapata kwa sababu ya ubabe wao.
7. Hutu tujamaa huwa hatukubali kushindwa, na kushindwa kwao ni kurudi nyuma kujipanga.
8. Hutambua wanyama wagonjwa na hutumia sana fursa hiyo kuwakamata hasa wale wakubwa kama nyati na twiga.
9. Ukiwaonesha damu ni kama umewaharibu akili hapo hawatajali ww ni nani, binadamu, simba , chui, nyati ukianguka ndio wanaridhika.
 
10. Ni wanyama ambao hutumia muda mfupi sana kuridhishana kimapenzi, dakika chache tuu Biashara imeisha na kibend juu.
11. Huwaficha watoto wao wasiwaone wawapo katika mahaba, cha ajabu watoto wao mwaka mmoja tuu nao huanza kufanya waliyokuwa wamefichwa sasa sijui wanajifunzia ndotoni.
12. Staili wanayotumia kula hata wanyama wanaokula nyama huishia kuwatizama tuu, na hakuna anayeweza kuwasogelea hata kama ana njaa, fisi huwa anachekaa weeee mpaka anaamua akafanye kazi nyingine.
13.wakishiba muda wao mwingi hutumia katika michezo, mfano kupigana , kukimbizana nk.
 
14. Kachezee chochote alichonacho Ila ukitaka ubaya naye kaguse watoto wake na kama kamoja kambeya kapige kelele, jicho utalopigwa litasadifu unachokwenda kufanywa.
15. Jike hupandwa na dume mbabe, hivyo wanyonge wa mwisho huenda kutafuta majike katika koo zingine na huo huweza kuwawinda mwanzo wa kuanzisha jamii yao mpyaa.
 
UKIKUTANA NAO UFANYE NINI ****************
Inasemekana viumbe hawa pamoja kwamba ni wapenzi wa nyama lakini hawanaga neno na mwanadamu, humuheshimu kama mbwa anaowafuga wanaomuheshimu, sasa basi heshima unayopewa itumie vizuri, sio unaanza kuleta tabia zetu za kiswahili ukiona mbwa unaokota jiwe na kumtupia, hawa jamaa hawapendagi dharau, lakini pia hakikisha hauna sehemu inayovuja damu kwani wakiisikia tuu wafyaa ! wakati huo endelea kufanya jitihada za kupotea maeneo hayo, maana ni binadamu tuu ndiyo amepewa ufahamu timilifu japokuwa naye hujichetua inapobidi.
 
Wanyama hawa wapo wengi sana nasikia ukiweka utaratibu mzuri wa kutembelea mbuga zetu bila kukata tamaa, kuna siku unaweza pewa nyongeza mbwa mwitu au fisi maana tunao wengi sana hapa Bongo, pitia mbuga zetu ukajionee timbili la wababe hawa wa mji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…